Breaking News

Your Ad Spot

Feb 28, 2014

MWIGULU, MGOMBEA WA CCM KALENGA, WASHIRIKI MAZISHI YA WANANCHI WATATU WALIOKUFA KWA AJALI YA GARI JIMBO LA KALENGA, IRINGA


 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba, akishiriki katika mazishi ya mmoja wa vijana watatu waliokufa baada ya kupata ajali ya gari katika Mlima Ukwasi, lilikuwa likienda Kijiji cha Tungamalenga kupeleka biashara ya maji. Mazishi hayo yalilifanyika jana katika Kijiji cha Kidamali Kata ya Mzihi, Jimbo la Uchaguzi la Kalenga, Iringa Vijijini leo
 Mgombea wa CCM katika Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa akishiriki katika maziko ya mmoja wa vijana waliokufa kwenye ajali hiyo. Waliokufa kwenye ajali hiyo ni dereva Nyagile Luvanda,Sabasaba Kuzungola na Ansikali Chengula.CCM imetoa ubani kwa wafiwa sh. mil. 1 na kuahidi kuwasomesha watoto wa waifiwa.
 Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga kupitia tiketi ya CCM, Gobfrey Mgimwa  (wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya vijana wa Kijiji cha Kidamali alipokwenda kuwafariji wafiwa wa misiba hiyo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba (aliyevaa kombatii), akiwa na Mgombea Ubunge Kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (kulia kwake), na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu walipofika Kijiji cha Kidamali.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa akisalimiana na baadhi ya vijana katika Kijiji cha Kidamali.
 Baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu wakilia na  baada ya kuona magari yaliyobeba miili katika Kijiji cha Kidamali.
 Sehemu ya waombolezaji
 Jeneza lenye mwili wa mmoja wa vijana walikufa kwenye ajali hiyo ukiwasili eneo la maziko
 Mwili mwingine ukiwasili eneo la makaburi katika Kijiji cha Kidamali
 Sasa ni wakati wa maziko. Moja wa wana CCM akishiriki katika maziko hayo
 Nchemba na Mgimwa wakiwa katika maziko hayo
 Wanahabari wakiwa katika maziko hayo
 Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kidamali, walioshiriki mazishi ya vijana hao, wakisoma vipeperushi vilivyokuwa vikisambazwa na wafuasi wa Chadema wakati maziko ya vijana hao yakiendelea katika makaburi kwenye Kijiji cha Kidamali leo.


 Ulinzi wa askari ukiwa umeimarishwa wakati wa maziko ya vijana hao.
Gari lililopata ajali na kusababisha vifo vya vijana hao. Imetayarishwa na Kamanda Richard Mwaikenda

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages