Breaking News

Your Ad Spot

Mar 1, 2014

DC HANANG AWAKUTANISHA VIJANA 316 KATIKA WILAYA HIYO, WAUNDA SACCOS YAO


HANANG, Tanzania
MKUU wa wilaya ya Hanang Christina Mndeme amewakutanisha vijana 316 wa wilaya hiyo na kuunda SACCOS yao, katika kutelekeza sera ya CCM ya kuwakomboa vijana kichumi na kuondokana na umaskini na pia kuwaondoa vijana kutojihisisha na shughuli ambazo hazina tija kwao na taifa.

Saccos hiyo ambayo tayari imesajiliwa kwa jina la Hanang Vijana  inawanachama wapatao 269 katika wenye ikundi vitano vya ufugaji kuku wa kienyeji, ufyatuaji wa matofali kisasa kwa teknolojia ya hydroform, bodaboda,  ufugaji nyuki na kilimo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema leo kwamba, Saccos hiyo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni wilayani Hanang na

Waziri wa Habari, Vijana, Utamadu7ni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara waziri wa habari, vijana.

"Vijana wa wilaya hii wamefurahia muungano huu kwani wamesema ni kwa mara ya kwanza tangu wilaya imeundwa kwa mkuu wa wilaya kuwaunganisha vijana bila kujali itikadi zao wala dini wa jinsia", alisema Mkuu huyo wa nwilaya

Alisema vijanahao wameishukuru sana serikali kwa mpango huo wa kwaunganisha na wameahidi kushiriki kikamilifu katika shushuli za kiuchumi na kushirikiana na serikali.

Mkuu huyo alisema Saccos hiyo inaundwa na vija wote kuanzia wenye elimu ya Chuo Kikuu mpaka darasa la saba na

ambao hawakwenda shule na kauli mbiu yao ni: "Juhudi za vijana ni ukombozi wa taifa- Hanang amani na maendeleo".

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages