Meneja
Uhusiano wa Transevents Makerting, Ednah Rebeccah akitoa maelezo kwa washindi
wa shindano la Dereva Makini Sabreena Munir na Vincent Bern ambao walipatikana
kwa kujibu maswali kupitia ukurasa wa facebook wa kampuni hiyo yaliyolenga
kujua ufahamu wao katika kuzingatia usalama kwenye vyombo vya usafiri.
Mshindi
wa shindano la 'Maswali ya Usalama Barabarani' Sabreena Munir akipokea
kuponi ya kwenda kula chakula cha usiku kwenye mgahawa wa Akemi unaozunguka (Akemi
revolving restaurant)
Mshindi
wa shindano la 'Maswali ya Usalama Barabarani' Vincent Bern akipokea
kuponi ya kwenda kula chakula cha usiku kwenye mgahawa wa Akemi unaozunguka (Akemi
revolving restaurant)
Meneja
Uhusiano wa Transevents Makerting, Ednah Rebeccah akitoa maelezo kwa washindi
wa shindano la Dereva Makini Sabreena Munir na Vincent Bern ambao walipatikana
kwa kujibu maswali kupitia ukurasa wa facebook wa kampuni hiyo yaliyolenga
kujua ufahamu wao katika kuzingatia usalama kwenye vyombo vya usafiri.
Washindi
hao wamepata zawadi ya chakula cha usiku wakiwa na wenza wao kwenye mgahawa Akemi
unaozunguka (Akemi revolving restaurant), pamoja na vinywaji na usafiri.
Meneja
Uhusiano wa Transevents Makerting, Ednah Rebeccah anasema lengo la kutoa
shindano hilo siku ya wapendanao ni kuihimiza jamii kuitumia siku hiyo kwa
kukumbushana mambo ya usalama barabarani.
Anasema
kuwa ajali za mara kwa mara zinazotokana na kutozingatiwa kwa sheria za usalama
kwenye vyombo vya usafiri zimechukua maisha ya watu wetu wa karibu na wapendwa
wetu.
“Ni
vyema kutumia siku hii kukumbushana namna ya kuzingatia usalama kwenye vyombo vya
usafiri, ni vyema kuhakikisha unazingatia usalama maana kusafiri na kufika
salama uendako ni zawadi kubwa sana ya Valentine” anasema Edna
Transevents
Marketing imeanzisha kampeni ya dereva makini ambayo inalenga kuhamasisha madereva
nchini kuendesha kwa kufuata sheria za barabarani na kuwa makini katika uendeshaji
wao.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269