Breaking News

Your Ad Spot

Feb 14, 2014

UN: RADIO NYINGI HAZINA HABARI ZA USAWA WA KIJINSIA

DSC_0010
Mshehereshaji Meneja wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania( MCT), Bw. Allan Lawa, akiwakaribisha wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma. Maadhimisho hayo yameandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na kufadhiliwa na UNESCO.
Na Mwandishi Wetu, Moblog Tanzania, Dodoma
UMOJA wa Mataifa umesema kwamba bado redio nyingi duniani ziko nyuma katika kuhabarisha habari za usawa wa jinsia na sauti za wanawake na wasichana hazipati nafasi ya kutosha katika matangazo ya kila siku katika vyombo vingi vya habari.
Akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw, Ban Ki-Moon na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Irina Bokova, katika maadhimisho ya siku ya Radio Duniani jijini Dodoma, Afisa Habari wa umoja wa Mataifa, Bi Usia Nkhoma Ledama amesema mbaya zaidi katika bodi za mashirika ya vyombo vya habari wanawake ni robo tu ya wanabodi.
“Ninavihimiza vituo vya redio kuwatambua kwa usawa wanawake kama wafanyakazi na kama wasikilizaji wake,”
“Maadhimisho ya mwaka huu yanatukumbusha wajibu wa watangazaji wa redio duniani kote kuipaza sauti ya wanawake na kuthamini nafasi ya wanawake katika mashirika ya utangazaji,” akisoma taarifa hiyo
Bi Usia akisoma taarifa hiyo amesema Radio pia inaweza kusaidia sana kumaliza unyanyapaa dhidi ya wanawake na programu zisizozingatia usawa wa kijinsia kwa wote.
DSC_0019
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akisalimiana na Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco, Mama Rose Haji Mwalimu meza kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga.
Amesema kwenye hotuba hiyo ya wakuu wa Umoja wa Mataifa kwamba hii ni fursa kwao wote, kusherehekea Siku Ya Radio Duniani kwa kuwatambua wanawake na kufanya yale yaliyo ndani ya uwezo wao kuzilea sauti mpya za kesho.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi Irina Bokova amesema na ninanukuu; Katika Siku ya Redio Duniani, tunaadhimisha chombo ambacho kinategemewa zaidi na watu wengi, wanaume kwa wanawake, duniani kote. Redio huwapa sauti wale wasio na sauti, husaidia kuelimisha watu wasio na elimu, na inaokoa maisha wakati wa majanga.
Akisoma taarifa hiyo amesema ikiwa ni chachu ya uhuru wa kujieleza na ushirikishwaji wa wengi, redio ni muhimu katika kujenga jamii yenye uelewa na kukuza heshima na uelewano baina ya watu.
DSC_0036
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari (MCT), Bw.Kajubi Mukajanga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi.
Ujumbe huo wa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO ulisisitiza kwamba Radio ni muhimu zaidi katika kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.
“Tangu wakati wa watendaji waanzilishi mwanzoni mwa karne ya 20 hadi hawa wa sasa wanaoripoti kutoka kwenye maeneo yenye vita, wanawake wamefanya kazi kubwa katika ukuaji wa redio,Kama waandishi wa habari wa kiraia, maripota, watengenezaji vipindi, mafundi, na watu muhimu wanaofanya maamuzi, wanawake wanafanya kazi katika kila ngazi ya sekta ya utangazaji kuhakikisha ubadilishanaji huru wa maoni, habari na mawazo kupitia masafa,” ilisema taarifa hiyo.
Bi Usia amesema kupitia ujumbe huo kwamba ni kwa sababu hiyo UNESCO inafanya kazi duniani kote kuendeleza radio kama chombo huru na kinachoshirikisha watu wengi kwa ajili ya wanaume na wanawake, na kutengeneza mazingira salama zaidi kwa waandishi wa habari wote, kwa kutambua kwa namna ya pekee vitisho kwa waandishi wa habari wanawake.
DSC_0120
Pichani juu na chini ni Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na wadau wa sekta ya Habari nchini kwenye maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr.Rehema Nchimbi ambaye aliwaasa waandishi kutangaza vipindi vyenye manufaa kwa jamii ili kusaidia kusukuma maendeleo.
“Tungependa kusikia vipindi vya maendeleo zaidi katika redio kuliko vipindi vya muziki,”alisema
Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari (MCT)Kajubi Mukajanga alisema maadhimisho hayo yamewashirikisha washiriki kutoka nchi nzima na yanalenga kuwakumbusha wajibu watangazaji wa redio juu ya nafasi ya radio katika kuelimisha jamii.
DSC_0103 DSC_0157
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama, akisoma Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi Irina Bokova katika Maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani.
DSC_0288
Mchokonozi wa Mada na Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu akiwasilisha mada inayosema kutumia fursa ya Redio kukuza usawa wa Kijinsia na kuwawezesha Wanawake katika Uongozi.
DSC_0181
Meneja Machapisho, Utafiti na Uhifadhi Hati wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. John Mireny, akitoa maelezo mafupi kuhusu machapisho mbalimbali ya baraza hilo yanayotoa mafunzo mbalimbali ya tasnia ya habari.
DSC_0218
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akizindua machapisho ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwenye maadhimisho ya siku ya Redio Duniani. Kushoto ni Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu na Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari (MCT), Bw.Kajubi Mukajanga.
DSC_0225
DSC_0045
Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Habari, Watangazaji na waandishi wa Redio za Jamii nchini wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma.
DSC_0052
DSC_0024
DSC_0066
DSC_0063
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani.
DSC_0060
Wadau wa UNESCO na MCT.
DSC_0323
Baadhi ya waandishi wa habari wa Redio za jamii nchini na wadau wa sekta ya habari wakichangia maoni wakati wa majadiliano ya kuzungumzia changamoto zinazozikabili redio za jamii nchini.
DSC_0321
DSC_0274
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Sekta ya habari walihudhuria maadhimisho ya siku ya Redio duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages