Na Mwandishi wetu
BODI ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imemshauri Waziri wa Maliasili
na Utalii, Lazaro Nyalandu kumuondoa kazini Murugenzi Mtendaji wa Bodi
hiyo, Dk. Aloyce Nzuki kutokana na utendaji usioridhisha.
Katika kikao cha pamoja kati ya bodi hiyo na Nyalandu pamoja na Naibu
wake Mahamoud Mgimwa, Katibu Mkuu Maimuna Tarishi na Naibu Katibu
Mkuu, Selestine Gesimba, waziri aliridhia uamuzi wa bodi, ambapo
alisema Dk. Nzuki atapangiwa kazi nyingine.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Charles Sanga, ndiye alitangaza uamuzi huo
akisema ni vema Dk. Nzuki akaondolewa kwa sababu hawataweza kufanya
naye kazi.
Alisema utaifa na uzalendo ni kiti kizuri kwa watanzania na pia bodi
yao inafanya kazi kwa ufanisi kwa ajili ya wananchi na madaraka ni
dhamana, hivyo hawataweza kufanya kazi na Dk. Nzuki.
Nyalandu alisema aliridhia uamuzi huo baada ya kupokea barua kutoka
Bodi ambayo ilisainiwa na wajumbe hao ikimshauri amuondoe Dk. Nzuki
kutokana na kutokuwa na imani naye.
Baada ya kuridhia uamuzi huo aliiagiza bodi kuitangaza nafasi hiyo kwa
watanzania wenye sifa duniani kote na waombe kazi hiyo ndani ya siku
21 kuanzia leo.
Aidha, Nyalandu alisema nafasi hiyo kwa sasa itakaimiwa na Mkurugenzi
wa Masoko, Devota Mdachi hadi hapo mchakato wa kumpata mkurugenzi
utakapokamilika.
Your Ad Spot
Mar 24, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269