Breaking News

Your Ad Spot

Mar 27, 2014

KINANA AWATEKA KIGAMBONI, MGOGORO KUHUSU UJENZI MJI WA KISASA ENEO HILO AAHIDI KUUPELEKA VIKAO VYA NGAZI ZA JUU CCM

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana, Machi 26, mwaka huu, katika eneo la Kigamboni, wiulayani Temeke akiwa katika ziara yake mkoani Dar es Salaam, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua na kugagua utekelezaji wa ilani ya Chama. 
   Akizungumza na wananchi wa Kigamboni, Kinana ameahidi kulichukua suala linaloonekana kuzua mgogoro mkubwa baina ya wananchi na serikali la ujenzi wa mji wa kisasa wa Kigamboni, Kinana ameahidi kulifikisha kwenye vikao vya ngazi ya juu kabisa vya CCM kwa uamuzi wa uhakika na wa kudumu.
  Kinana amesema, baada ya kulifikisha kwenye vikao vya juu ya CCM atarejea tena Kigamboni kuzungumza na wananchi ili kuwapa majibu sahihi.
   "Hapa ni lazima tujue, wazo la kubuniwa mradi huu lilianzishwa na nani, kwa lengo na maslahi gani, na wananchi ninyi mnaoishi hapa mlihusishwa kwa kiwango gani kuhakikisha mchakato mzima unakuwa halali kwa mujibu wa sheria za nchi", alisema Kinana.
 
Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Kinana alipoowahurubia katia mkutano huo
 Kassim Abdallah mkazi wa Vijibweni Kigamboni akitoa hoja zake mbele ya Kinana kuhusu mradi huo
 Khalfan Iddi ambaye alikuwa kada wa CUF akikabidhi kadi yake kwa Kinana baada ya kuridhiwa na hotuba ya katibu mkuu huyo kwenye mkutano huo wa Kigamboni
 Kinana akiagana na wananchi baada ya mkutano
Kinana akiongdoka uwanjani baada ya mkutano. Kulia ni mwenyekiti wa CCM Temeke, Yahya Sikunjema. Picha zote na Bashir NKoromo wa theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages