(Picha na Maelezo-Dodoma)
(Na Magreth Kinabo- MAELEZO,Dodoma)
Umoja wa Watumiaji wa Ardhi umewataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kuanza kuifanya kuichambua Rasimu ya Katiba Mpya kama walivyotumwa na wananchi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuacha kufanya kampeni za kufatuta madaraka kuliko kusimamia maslahi ya wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa umoja huo , Dk. Maselle Maziku katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma .
Amesema umoja huo utafanya kazi ya ya kuhakikisha unatetea haki za wakulima ,wafugaji na wavuvi katika mchakato wa kujadili Rasimu ya Katiba Mpya.
“ Tunawataka wanasiasa watambue kwamba katikaBunge hili, hatukuja kufanya mabishano yasiyokuwa na mwisho na badala yake tunataka tuanze kuifanya ile kazi ambayo wananchi wametutuma ya kupitia na kuichambua Rasimu ya Katiba,” alisema Dk. Maselle .
Aliongeza kuwa umoja huo , umegundua kwamba makundi ya wanasiasa yanavuruga mchakato wa Bunge hilo kwa kuendekeza misimamo yao ya kiitikadi na kusahau azma iliyowaleta ya kuhakikisha Watanzania wanapata Katiba Mpya isiyokuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa.Hivyo umeshoshwa na hali ya Bunge hilo kuonekana kuwa ni sehemu ya makundi ya wanasiasa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269