Breaking News

Your Ad Spot

Mar 10, 2014

KUTOKA BUNGE LA KATIBA LEO MJINI DODOMA

Mjumbe wa bunge Maalum la Katiba Bw.  Augustino Mrema akimweleza jambo Mjumbe mwenzie Bw. Islaim Aden Rage leo Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalumla Katiba na Wajumbe wa kamati ya kuandaa rasimu ya kanuni zitakazotumika katika Bunge maalum la Katiba Bw. Prof. Costa Mahalu (Kulia) na Tundu Lissu wakielekea katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge maalum la katiba Bw. Hamadi Rashidi (kushoto) Juma Alawi (katikati) na Thumwein Thuwein wakielekea katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge maalum la katiba Bw. Ally Kessy akiwaeleza jambo jambo Wajumbe wenzie Bw. Edward Lowassa (katikati) na Almas Maige ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta (kulia) akimweleza jambo Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.
Mjumbe wa bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kuandaa rasimu ya kanuni zitakazotumika katika Bunge maalum la Katiba Bw. Prof. Costa Mahalu akiwaeleza jambo wajumbe wa bunge hilo wakati wa semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma. (PICHA NA HASSAN SILAYO- MAELEZO)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages