Wananchi wa mji mdogo wa Kalenga, katika Kata ya Kalenga, Iringa Vijijini, wakimshangilia kwa bashasha mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa, alipokuwa akiwaaga, baada ya kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni katika kijiji hicho leo.
Wananchi wa mji mdogo wa Kalenga, Iringa Vijijini wakiwa katika hoihoi na nderemo kumkaribisha mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, alipofika kuhutubia mkutano wa kampeni katika eneo lao leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula akihutubia mkutano wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, uliofanyika katika mji mdogo wa Kalenga, Iringa Vijijini leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, akimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Godfrey Mgimwa, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Kalenga, Iringa Vijijini .
Mgombea ubunge jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM Godfrey Mgimwa, akihutubia mamia ya watu kwenye mkutano wa kampeni leo katika mji mdogo wa Kalenga, Iringa Vijijini.
Mgimwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu, wakisalimia wananchi baada ya mkutano wa kampeni katika mji mdogo wa Kalenga, Iringa Vijijini leo.
Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa, akiwa amebebwa na Wananchi alipowasili kuhutubia mkyutano wa kampeni katika kijiji cha Ipamba, Tosamaganga
Sista Paula Msambwa mwenye umri wa miaka 73, akimbusu kwa furaha, mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Godfrey Mgimwa, mgombea huyo alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Ofisi ya CCM Tosamaganga, Iringa Vijijini leo. Sista Paula alisema, aliwahi kuwa mwalimu wa Baba wa mgombea huyo, Marehemu Dk. William Mgimwa miaka 50 iliyopita katika shule ya Tosamaganga.
Sista Paula Msambwa akimtakia kila la kheri ikiwemo kushinda katika uchaguzi, mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa, alipopewa fursa ya kuzungumza kwenye mkutano huo.
Mgombe ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, akihutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Ipamba, Tosamaganga leo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akihutubia mkutano wa kampeni kwenye kijiji hicho.
Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akipokea kadi ya Chadema
kutoka kwa Said Omary Mbilinyi ambaye amerudi CCM kwenye mktano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye kijiji hicho.
Kada wa CCM kutoka Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM, Mtela Mwampamba
akihutubia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Kijiji cha Ipamba, Tosamaganga, leo na kuwataka wananchi kutambua kuwa huduma ambazo huwa wanaziona kwa kupelekwa kwao na serikaloi zina uhusiano mkubwa na CCM.
Katibu wa CCM
Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Tosamaganga wakati wa kumnadi mgombea wa kiti cha ubunge kupitia CCM, Godfrey Mgimwa.
Hizi ni shamrashamra za wananchi zilizohanikiza wakati mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la kalenga, Godfrey Mgimwa, alipowasili katika kijiji cha Ipamba, Tosamaganga
Wafanyabiashara katika Kijiji cha Ipamba, Tosamaganga wakiwa wamecha vibanda vyao vya biashara na kwenda kumsikiliza mgombea ubunge jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM, Godfrey Mgimwa alipohutubia katika kijiji hicho leo
Helen Msambwa, wa kijiji cha Ipamba, Tosamaganga, akiandaa samaki, huku akifuatilia kwa karibu hotuba ya mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Kalenga , Mgimwa alipohutubia kwenye eneo hilo leo. Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog
Your Ad Spot
Mar 10, 2014
Home
Unlabelled
CCM YATIKISA KATA YA KALENGA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA
CCM YATIKISA KATA YA KALENGA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269