Breaking News

Your Ad Spot

Mar 11, 2014

WATANZANIA WAHIMIZWA KUJISOMEA MAJARIDA

 Cosmas Njingo-afisa habari na mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro akichangia mada.
  Zadock Kitomary-Mkulima bora mara mbili mfululizo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mkoani Arusha akitoa mada.


Ayubu Nnko-Msimamizi wa Jarida kwa upande wa Tanzania akitoa mada katika Semina hiyo.

  Coroline Nyakundi- Meneja Mradi The Organic Farmer& jarida la Mkulima mbunifu akitoa mada.

John Cheburet-Mtayarishaji wa vipindi vya Redio kutoka jarida la Mkulima mbunifu .
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali na Mafunzo katika semina hiyo
******
Na Arusha yetu Blog
IMEELEZWA kuwa Watanzania ni wavivu wa kusoma Majarida mbali mbali yanayoweza kuwaongezea upeo ukilinganisha na nchi zingine.

Hayo yamebainishwa na Mmoja wa maafisa wa Jarida la Mkulima Mbunifu, Caroline Nyakundi kutoka Nchini Kenya, wakati akizungumza katika mafunzo ya waandishi wa habari za kilimo na wataalamu wa kilimo yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Arusha Crown ya Mjini hapa.

Ameongeza kuwa kunatofauti kubwa ya Mwitikio wa kusoma machapisho kati ya Raia wa Tanzania ukilinganisha na Kenya ambako imeelezwa kuwa wanauhitaji mkubwa wa kujifunza mbinu mpya za kilimo tofauti na Watanzania ambao hawana uhitaji wa kusoma na kutaka kujua zaidi.

Akieleza Mikakati ya Jarida la Mkulima Mbunifu mmoja katika ya Maafisa wa Jarida hilo, Caroline Nyakundi kutoka Nchini Kenya, amesema tangu kuzinduliwa kwa jarida hilo Juni,2011 limeonesha mwitikio mkubwa kutokana na kupata taarifa nyingi kutoka kwa wakulima wakilihitaji ili kujua zaidi habari za Kilimo.

Amesema Jarida hilo limelenga zaidi maoni na mahitaji ya Mkulima kutokana na mawazo yao ambayo wamekuwa wakiyatoa katika jarida hilo mara kwa mara jambo linaloonesha Mkulima kufikiwa na Jarida hilo na kwa wakati.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages