Breaking News

Your Ad Spot

Mar 7, 2014

STARS KUREJEA NCHINI LEO MCHANA KUTOKA NAMIBIA

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kurejea nchini leo (Machi 7 mwaka huu) saa 12.45 jioni kutoka Windhoek, Namibia kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA.

Taifa Stars ambayo katika mechi hiyo dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ilitoka sare ya bao 1-1 itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.15 mchana kwa ndege ya South Africa Airways.

Timu inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager baada ya kuwasili itakwenda hoteli ya Accomondia kwa ajili ya chakula cha mchana na baadaye kuvunja rasmi kambi yake.

Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer

Tanzania Football Federation (TFF)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages