Breaking News

Your Ad Spot

Mar 24, 2014






TBL YAKABIDHI KISIMA CHA MAJI MJI MDOGO WA TUNDUMA


Mkurugenzi
wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa
Wilaya ya Momba Abiud Saideya  akiwa na Meneja Matukio Kampuni ya Bia
Tanzania  TBL Kanda ya nyanda za juu kusini Claud Chawene wakikata utepe
kwa pamoja kuzindua kisima hicho cha Maji


Mkurugenzi
wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa
Wilaya ya Momba Abiud Saideya akiongea na wafanyakazi wakituo cha Afya
Tunduma mara baada ya kukabidhiwa kisima hicho na TBL


Afisa
uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja
kati ya Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa
kurudisha fadhila kwa Watanzania.




 Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma Elias Cheyo akitoa neno la shukrani kwa TBL


Baadhi ya wafanyakazi na wananchi wa mji wa Tunduma wakimsikiliza mgeni rasmi 


Diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka akiwashukuru kampuni ya Bia TBL kwa msaada wa kisima hicho


Afisa mipango Mji wa Tunduma Augustino Ngetwa akisoma taarifa fupi mbele ya mgeni rasmi




Mkurugenzi
wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa
Wilaya ya Momba Abiud Saideya  akiwa na Meneja Matukio Kampuni ya Bia
Tanzania  TBL Kanda ya nyanda za juu kusini Claud  Chawene wakielekea
eneo la makabidhiano ya kisima hicho 




Mkurugenzi
wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa
Wilaya ya Momba Abiud Saideya  wakipeana mikono Meneja Matukio Kampuni
ya Bia Tanzania  TBL Kanda ya nyanda za juu kusini Claud
 kuashiria kukabidhiwa kwa kisima hicho


Mkurugenzi
wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga wakipongezana na
mwenyekiti wa Halmashauri  ya mji  mdogo wa Tunduma Elias Cheyo mara
baada ya kukabidhiwa kisima hicho








Kituo cha Afya Tunduma















Kampuni ya
Bia Tanzania imetoa msada wa kisima cha maji kwa ajili kituo cha Afya Tunduma
chenye thamani ya shilingi milioni 24 chenye uwezo wa kutoa lita 5000 kwa saa.

Afisa
uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja kati ya
Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa kurudisha
fadhila kwa Watanzania.

Malulu
amesema kampuni yake imetenga jumla ya shilingi milioni 450 kwa ajili ya miradi
mbalimbali ya maendeleo nchini kwa kipindi cha mwaka wa fedha yenye nia ya
kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Naye Afisa
mipango Mji wa Tunduma Augustino Ngetwa amesema mradi huo utasaidia kumaliza  tatizo la maji hivyo kuwa faraja kwa
wagonjwa wanaotumia kituo hicho ikiwa ni pamoja na raia wa nchi jirani ya
Zambia.

Mkurugenzi
wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya
Momba Abiud Saideya  amesema kuwa
watahakikisha wanautunza mradi huo ili uwe na manufaa kwa kizazi cha sasa na
kijacho .

Aidha Diwani
wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka ameshukuru Kampuni hiyo kwa kutoa mradi huo
na hivyo kuwataka wahudumu kuitunza miundo  mbinu  ya maji. 

Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma Elias Cheyo ameitaka
kampuni ya bia kupanua wigo wa kusaidia Nyanja nyingine kama vile elimu ili
kufanya mji wa Tunduma kuwa na maendeleo zaidi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages