Breaking News

Your Ad Spot

Mar 23, 2014

DIWANI AANGUA KILIO MBELE YA RIDHIWANI KIKWETEBAADA YA MKANDARASI KUCHELEWESHA MRADI WA MAJI


 Diwani wa Kata ya Kimange, Hussein Hading'oka akiangua kilio mbele ya wananchi na mgombea ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia CCM, Ridhiwani Kikwete baada ya kukerwa na kitendo cha mkandarasi wa maji kuchelewesha Mradi wa maji katika kata hiyo. Tukio hilo lililtokea akielezea utekelezaji wa ilani ya chama hicho wakati wa mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Pongwe Kiona leo.

 Diwani Hading'oka akifutwa machozi na mmoja wa wanakijiji  cha Pongwe Kiona leo.



 Ridhiwani akimsikiliza kwa makini Mzee wa Kijiji cha Changarika Juma Ramadhan, Kata ya Mbwewe  wakati wa kampeni hizo.

Ridhiwani (katikati)  akiwa na  Mkurugenzi  wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma Pinto pamoja na mmiliki wa Blogu ya Wananchi, William Malecela wakati wa kampeni za jimbo la Chalinze ambapolo Ridhiwani anagombea.

 Ridhiwani akijadiliana jambo na Pinto katika Kijiji chA Kimanga leo

 Kwaya ya Kijiji cha Kimange, Kata ya Kimange wakitumbuiza kwa furaha wakati wa kampeni za CCM Jimbo la Chalinze

 Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiungana na wananchi wa Kijiji cha Pongwe Kiona kumuombea aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Chalinze, marehemu Said Bwanamdogo wakati wa mkutanio wa kampeni leo.

 Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto) akiungana na baadhi ya wananchi walionyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kumpigia kura April 6 mwaka huu.

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho Mkoa wa Mtwara, akiuhutubia kumnadi Ridhiwani Kikwete katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Pongwe Kiona leo

 Ridhiwani Kikwete akijinadi katika Kijijic cha PongweKiona leo.

 Mzee Omari Abdallah (80) akimsikiliza kwa makini mgombea ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia CCM,Ridhiwani Kikwete aliyekuwa akijinadi katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Pongwe Kiona leo.

 Ridhiwani Kikwete akizungumza na baadhi ya vijana wa Kijiji cjha Pongwe Mnazi baada ya kumalizika kwa mkutano kijijini hapo leo.

 Ridhiwani akiombewa dua baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Pongwe Mnazi leo

 Ridhiwani Kiwete akikagua majengo ya shule ya MsingiKikwazu Kata ya Kimange leo.

 Wananchi wakinyoosha mikono kukubali kumpigia kura Ridhiwani Kiwete Aprili 6 mwaka huu.

 Ridhiwani akisalimiana na baadhi ya wazee katika Kijiji cha Kifulete, Kata ya Kimange

 Ridhiwani akiteta jambo na Mariam Khami ambaye ni mlemavu wa macho katika Kijiji cha Kifulete baada ya kumaliza mkutano wa kampeni leo

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akijadiliana jambo na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Changarika leo

Wasanii wa ngoma ya Sero wakicheza mbekle ya Ridhiwani Kikwete wakati wa Mkutano wa Kampeni katika Kijiji cha Changarika , Katea ya Mbwewe leo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages