DODOMA, Tanzania
Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Samwel Sitta leo, ametangaza majina ya wenyeviti
na makamu wenyeviti wa Kamati za bunge hilo.
Majina
hayo yametangazwa na Mwenyekiti huyo
baada ya uchaguzi wa viiongozi hao uliofanyika (jana) Machi 24 , mwaka 2014 mjini Dodoma .
Mwenyekiti
huyo aliyataja majina hayo katika Kamati
ya Uandishi Mwenyekiti Andrew Chenge,
Makamu wake ni Mgeni Hassan Juma. Kamati ya Kanuni Mwenyekiti ni Pandu Ameri
Kificho, Makamu wake ni Dkt. Susan Kolimba. Kamati Na. 1 Mwenyekiti ni Ummy Ally Mwalimu, na Makamu wake ni Prof. Makame
Mbalawa.
Wengine
waliochaguliwa katika Kamati Na. 2 Mwenyekiti
ni Shamsi Vuai Nahodha, Makamu wake ni Shamsa Mwangunga.Kamati Na. 3 Mwenyekiti ni Dkt. Francis Michael, Makamu wake ni Fatma MussaJuma.
Mhe.
Sitta alisema waliochaguliwa katika Kamati Na. 4 Mwenyekiti ni Christopher Ole-Sendeka, Makamu wake ni Dkt. Sira Ubwa Mamboya, Kamati Na. 5 Mwenyekiti
ni Hamad Rashid Mohamed Makamu wake ni Assumpter Mshama.
Kamati
Na. 9 Mwenyekiti ni Kidawa Hamidi Saleh,Makamu wake Wiliam Ngeleja,Kamati Na. 10 Mwenyekiti ni Anna Abdallah, Makamu wake ni Salmin Awadh Salmin.Kamati Na. 11 Mwenyekiti
ni Anne Malecela, Makamu wake Hamad Masauni
na Kamati Na. 12 Mwenyekiti
Paul Kimiti na Makamu wake ni Thuwaybah E. Kisasi.
Wakati
huohuo , Sitta alitangaza wajumbe wa
Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum la
Katiba, ambao ni wenyekiti na makamu
wenyeviti wa kamati hizo wakiwemo wajumbe wengine watano aliowateua.
Wajumbe hao walioteuliwa na Sitta kuingia
katika kamati hiyo ni Fakharia Khamisi Shomari, Mary Chatanda, Profesa Ibrahim
Lipumba, Amon Mpanju na Hamad Abuu Juma.
Hata hivyo pamoja na majina hayo kutangazwa
Profesa Lipumba alisimama na katika nafasi hiyo .
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269