Na Mwandishi Maalum, New York
Documentary Tanzania; A Journey Within, ambayo wahusika wake wakuu ni Kristen Keeney dada wa kimarekani na kaka wa kitanzania Venance Ndibalema imekuwa kivutio kikubwa kwa watizamaji wengi na kujizoelea sifa kemkem.
Documentary hiyo imeanza kuoneshwa katika baadhi ya kumbi za senema hapa jiji New York Aprili 25 ambayo ilikuwa Malaria Duniani. Licha ya kuhudhuriwa na watizamaji wengi mwandishi wa habari hizi ambaye alikuwapo siku ya ufunguzi alishuhudia namna watizamaji hao walivyoguswa kiasi cha baadhi yao kutokwa machozi.
Ni documentary ambayo inawakutanisha wahusika wakuu wenye mila na tamaduni zinatofautiana, mmoja akitokea katika nchi iliyoendelea kwa kila kitu na familia yenye uwezo na kijana wa kitanzania kutoka nchi inayoendelea Tanzania.
Vijana hao wawili urafiki wako ulianzia kwenye uwanja wa mpira, urafiki uliopelekea kwa Kristen kumshawishi Vencance aje kutembelea Tanzania, na si kuishia katika majiji na miji mikubwa ya Tanzania, bali alitaka pia kwenda vijijini kujifunza na kama si kujionea maisha halisi ya mtanzania.
Ni Documentary ambayo kwa yeyote anayeitizima hutoka akiwa mtu mwingine na nikra tofauti. Documentary hii tofauti na nyingine ambazo wahusika huandikiwa mistari ya kukariri na maeneo ya kuingizia, hii inaonyesha uhalisia wa si tu wawahusika wakuu bali, maisha halisia ya mtanzania, ukarimu wao, upendo wao, raha zao, taabu zao, uvumilivu wao na kujituma kwao.
Ni maisha haya aliyoishi Kristen, ambayo siyo tu yamembadilisha mtizamo wake, lakini kwa maneno yake anasema amezaliwa upya.
Akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa watizamaji mwishoni mwa onesho ambalo limeongozwa na mshindi wa tuzo kadhaa za Emmy Award Sylivia Caminer. Kristen ansema.
“ Najijisi kuzaliwa upya , upendo na ukarimu walionionyesha watanzania wale, upendo wa kweli unaotoka moyoni, upendo ambao haukujali rangi yangu, wala ninatoka wapi, umenitia moyo sana, kiasi cha kuona kwamba kumbe mali na maisha mazuri bila ya upendo wa kweli hauna maana yoyote.
Kristen siyo tu alikwenda migombani na kukata mgomba wa ndizi na kuubeba kichwani, kumenya ndizi, kupika kwa kutumia kuni, kuchota maji mtoni, mto ambao maji hayo hayo yalikuwa yakitumiwa na mfugo huku wengine wakioga, lakini pia alikuwa mhanga wa malaria, ugonjwa uliomfanya alazwe kwa siku mbili na kupatiwa matibabu katika zahati moja huko Bukomba Vijiji.
Kuugua kwake malaria, na upendo wake kwa watanzania na kama vile kurejesha fadhila, Kristine na mshirika wake wameamua kufanya mambo mbalimbali ya kusaidia vita dhidi ya malaria.
Kwa mfano imeanzishwa ijulikanayo kama Malaika for life. Asasi hii hujishughulisha na uuzaji wa bangili, urembo ambao umetengenezwa na wanawake wa kitanzania. Kauli mbiu ya bangili hizi ni buy a bracelet, save a life. Kupitia mchango wa Malaika for life, michango hiyo imeweza kuokoa maisha ya watu 22,000 dhidi ya ugonjwa wa malaria.
Akiuguzumzia ugonjwa wa Malaria Kristen ambaye licha ya kuishi maisha ya kijiji lakini pia alipata fursa ya kuupanda Mlima Kimajaro hadi kileleni na vile vile kutembelea mbuga ya wanyama anasema, ugonjwa wa malaria unatibika.
“ Nimatumaini yetu kwamba mnaponunua tiketi ya kuja kuangalia documentary hii mnachangia katika kuokoa maisha ya mtu mmoja au mtoto mmoja michango tunayopata tunanunua dawa pamoja na vifaa vya kupimia na kugundua ugonjwa wa malaria kwa haraka na kwa muda mfupi” anasema Kristen.
Kwa upande wake, Venance anasema uamuzi wake wa kushiriki documentary hiyo ambayo itaonyeshwa hapa New York hadi Mei mbili na baada hapo itaonyeshwa katika majimbo mengine likiwamo la Los Angeles. Anaamini kwamba utasaidia sana kuokoa maisha ya watanzania wengi hususani katika eneo hilo la kupambana na malaria.
Washiriki wengi walijitokeza kuangalia documentatry hiyo ambayo tayari
imeshajizoelea sifa tele, washiriki wengi licha ya kuvutiwa ma maudhui
yake baadhi yao walijikuta wakitoa machozi baada ya kuguswa na
walichokiona
Washiriki wa onyesho wakiwa wamenyayua pipi kijiti ambazo ujumbe wake
ulikuwa "Malaria Sucks" ikiwa ni ishara yao ya kuunga mkono
mapambano dhidi ya Malaria
Your Ad Spot
Apr 28, 2014
Home
Unlabelled
DOCUMENTARY-TANZANIA; A JOURNEY WITHIN YAWA KIVUTIO, WENGI WAGUSWA NAYO
DOCUMENTARY-TANZANIA; A JOURNEY WITHIN YAWA KIVUTIO, WENGI WAGUSWA NAYO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269