Breaking News

Your Ad Spot

Apr 5, 2014

MAANDALIZI UCHAGUZI MDOGO CHALINZE TAYARI KWA ASILIMIA 95: TUME

BAGAMOYO, Tanzania
Jumla ya vituo 288 vinatarajiwa kutumika kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze wilaya  ya Bagamoyo mkoani Pwani kesho Jumapili, April 6, mwaka huu.

Akizungumzia hali maandalizi ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi jimboni hapo ambae pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Samuel salianga alisema taratibu zinazotakiwa zipo tayari kwa asilimia 95 na tayari vifaa vyote muhimu vimeshafika na kusambazwa katika vituo vya kupigia kura .


Alibainisha kwamba vituo vitakavyotumika  ni vile vilivyotumika katika uchaguzi uliofanyika mwaka uchaguzi mkuu 2010.


Aidha Salianga alisema kuwa Jumla ya vyama vitano CCM, CHADEMA, CUF, NRA na AFP vinatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huo na idadi ya wapiga ni 92,939.

Hata hivyo kwa upande mwingine tume ya Taifa ya uchaguzi -NEC imevitaka vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Chalinze kuhakikisha kuwa wanawatumia mawakala wanatoka eneo lenye vituo husika ili waweze kuwatambua wapiga kura wa eneo hilo.

Akizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva alisema sheria haikatazi vyama hivyo kuteua mawakala kutoka majimbo mengine ya uchaguzi lakini ni vema kuwateua wale wanaotoka eneo lenye wapiga kura wanaowafahamu.

Licha ya kuwepo kwa idadi hiyo ya waliojiandikisha katika daftari la kupiga kura lakini kuna wasiwasi wa wapiga kura kutofikia idadi hiyo kutokana na miundombinu  katika baadhi ya maeneo kuharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini.

Uchaguzi huo unafanyika kutokana na kifo cha aliyekua mbunge katika jimbo hilo Said Bwanamdogo aliyefariki Januari 22 mwaka huu. 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages