Breaking News

Your Ad Spot

Apr 26, 2014

MWEMBE ULIOPANDWA NA NYERERE NA KARUME SIKU YA SHEREHE ZA MUUNGANO, KATIKA BUSTANI YA IKULU YA DAR ES SALAAM, WATIMIZA MIAKA 50 LEO

Wakati wa Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili 1964, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Zanzibar Abeid Amaan Karume ambao sasa wote ni marehemu,  walipanda katika shimo moja miembe miwili mmoja kutoka Zanzibar na mwingine kutoka Tanganyika. Miembe hiyo imekuwa na kustawi pamoja na kufanya shina moja 'through grafting' .Leo hii mti huo wa mwembe umestawi vyema katika bustani ya Ikulu, Dar es Salaam, kama unavyoonekana leo Aprili 26, 2014 ambayo ni Siku ya miaka 50 ya Muungano.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages