Breaking News

Your Ad Spot

Apr 26, 2014

SHEREHE ZA MUUNGANO WA TANGANYIKA NBA ZANZIBAR ZAFANA TAIFA LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
 Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa mwendo wa aina yake wakati wa sherehe za miaka 50 ya Muungano.
 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
 Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
 Makomandoo wa JWTZ wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja matofali kwa kutumia kichwa na mikono.
 Baadhi ya silaha za kivita za JWTZ zikipitishwa mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa wa jeshi letu.
 Kikosi cha Wanamaji
 Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais katika maonyesho ya JWTZ Ndege yaliofanyika kwenye Kilele cha  Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.
 Askari wa kikosi cha mwamvuli akishuka kutoka angani ambako ilielezwa ni umbali wa futi 4500 kwenye uwanja wa Uhuru kwenye kilele cha miaka 50.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha mwamvuli .
 Maandamano ya Pikipiki.
 Matembezi maalum ya kusheherekea miaka 50 ya Muungano .
Watanzania waliotimiza miaka 50 leo, sawa na miaka ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wakirusha njiwa wakati wa kilele cha  maadhimisho hayo leo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages