Vijana wakiwa kwenye matembezi ya Uzalendo yalioratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Matembezi hayo ambayo yalianzia Ofisi ya CCM Wilaya ya Temeke hadi kwenye viwanja vya Maonyesho ya Mwalimu Nyerere vya sabasaba yalipokewa na Rais Dk. Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein.
Vijana wakionyesha ukakamavu huku wakidhihirisha Utanzania wao wakati wakiwa kwenye matembezi hayo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakishiriki matembezi hayoRais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida wakati wakisubiri mapokezi ya matembezi hayo
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Khamis akienda kukabidhi bendera ya Taifa kwa Rais Kikwete kwenye ukumbi wa PTA, mwishoni mwa matembezi hayo
Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage huku Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume, baada ya vijana walioshiriki matembezi kuwakabidhi picha hizo.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi baada ya kupokea matembezi hayo ya Vijana katika Ukumbi wa PTA kwenye Viwanja vya Maonyesho ya sabasaba vya Mwalimu Nyerere
Mamia ya watu wakimsikiliza Kikwete
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269