Breaking News

Your Ad Spot

Apr 9, 2014

ZIARA YA KINANA WILAYA YA KASULU MKOANI KIGOMA YAFANA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika leo, Aprili 9, 2014, kwenye stendi ya texi mjini Kasulu, akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi katika mkoa wa Kigoma
 Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye stendi ya texi mjini Kasulu. 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akuhutubia maelfu ya wananchi katika Kijiji cha Kurugongo, wilayani Kasulu mkoani Kigoma leo jioni. Kinana yupo katika ziara ya siku tano mkoani Kigoma kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua
 Mbunge wa Viti Maalum, Josephine Ngezabuke akihutubia wakazi wa kijiji cha Nyenge kata ya Kurugongo wakati wa mkutano wa Kinana uliofanyika kijijini hapo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakila karanga baada mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya michezo shule ya Msingi Nyenge kata ya Kurugongo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
 Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Abeid Karume aliyepo katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana mkoani Kigoma, akishiriki kucheza ngoma ya asili ya Waha iliyochezwa wakati wa mapokezi ya Kinana kwenye viwanja vya Stendi ya taxi Kasulu mjini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kituo cha stendi ya Taxi mjini Kasulu, na kusema kuwa CCM imedhihirisha kuwa na ukomavu kwenye demokrasia ya kweli na hali inavyoendelea hivi sasa wapinzani wameanza kupotea kabisa kwenye siasa hasa baada ya kushindwa vibaya kwenye chaguzi zilizopita hivi karibuni ambapo kwenye uchaguzi wa madiwani kati ya kata 27 walipata tatu, ubunge Kalenga na Chalinze wameanguka vibaya sana .
 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwapongeza wanachama walioamua kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Viwanja vya Texi mjini Kasulu mkoani Kigoma. Kulia ni Nahasoni Kigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF kata ya Rungwe mpya na Adolf Yanda aliyekuwa Katibu wa Chadema kwa wanafunzi wa chuo cha SUA, Zaidi ya wanachama 700 walijiunga na CCM katika mkutano huo na ule uliotangulia kufanyika Kijiji cha Kurugongo. Katika mkutano huo wa Kasulu mjini Kinana alitawazwa pia kuwa Mzee wa Kiha na kuvishwa mavazi rasmi ya kabila hilo ambalo ni pamoja na mgolole unaotokana na magome ya miti.
 Wananchi wakiwa wamembeba Diwani wa Kata ya Nyumbigwa Joseph Chalukula wakati wa mkutano wa Kinana uliofanyika kwenye Kijiji hicho leo, Aprili 9, 2014, ukiambatana na Katibu Mkuu huyo wa CCM kukagua mradi mkubwa wa maji kwa ajili ya Kijiji cha Nyumbigwa.
 Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa Kinana, uliofanyika leo katika Kijiji cha Rugongo, Kata ya Migunga, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Murugongo Kata ya Migunga, wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
 Mjumbe wa NEC, Daniel Nsanzugwanko (kulia) akimpa maelezo ya ziada Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, wakati Katibu Mkuu huyo alipokagua mradi wa maji wa Kijiji cha Nyumbigwa, wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Mradi huo unaotekelezwa na serikali kwa gharama ya sh. milioni 971 unatarajiwa kukamilika mapema mwaka huu.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kulia, wanaotembea) akikagua tangi la maji la mradi huo.
 Wananchi wa Kijiji cha Nyumbigwa wilayani Kasulu, wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, baada ya kukagua mradi wao wa maji katika kijiji hicho
 Katibu wa CCM wilaya ya Kasulu, Augustine Minja akizungumza wakati wa mkutano wa Kinana katika kijiji cha Nyumbigwa, wilayani humo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma,  Mohamed Nyawenga.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakiwa mbele ya Ofisi ya CCM wilaya ya Kasulu baada ya kuwasili leo. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages