Uchungu wa mwana aujuae mzazi lakini kwa Rapa 50 Cent
ameonekana kuupuzia msemo huo baada ya kukacha kuhudhuria mahafali ya
mtoto wake wa kwanza wa kiume ‘Marquise Jackson’ aliyekuwa akihitimu
masomo yake ya sekondari.
Akionekana kusikitishwa na kitendo alichofanya baba yake,
Marquise alitupia picha akiwa amekumbatiana na dada yake na kisha
kuandika ujumbe mzito uliosomeka
”Nilikuwa nahamu kubwa ya kumuona baba yangu katika mahafali
yangu lakini yeye hajaonyesha upendo. Dada yangu na mama daima wapo kwa
ajili yangu jua wazi kwamba wewe haupo. Nimeifanya bila wewe.
Licha ya Hitmaker wa 21Questions kutokutokea, Kijana wake
aliweza kupata kampani kutoka kwa mama yake ‘Shaniqua’, ndugu, jamaa,
marafiki pamoja na anko wake Jim Jones.
Hata hivyo 50 amekuwa akiripotiwa kutokuwa na maelewano
mazuri na mzazi mwenzake ikiwemo na kuripotiwa kumtumia mwanae ujumbe wa
vitisho ingawa baadae alikanusha vikali habari hizo na kudai kuwa
aliyekuwa akifanya hivyo ni mama wa mtoto huyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269