Washika mtutu wa jiji la London, klabu ya Arsenal hapo
jana iliweza kunyakua kombe la FA baada ya kuilowesha Hull City kwa
kipigo cha bao 3 kwa 1 katika mtanange uliochezwa kwenye dimba la
Emirates.
Mchezaji wa Arsenal Ramsey aliweza kuiwezesha
timu yake kuchukua ubingwa huo baada ya kufunga bao l dakika za
nyonngeza na kufanya matokea kumalizika kwa 3 – 2 dhidi ya Hull City.
Magoli ya Hull yakiwekwa kimyani kupitia James Chester na
Curtis Davies kabla ya kusawazishwa na Santi Carzola pamoja na Laurent
Koscienly huku goli la tatu na la ushindi likifungwa na Aaron Ramsey .
Inakumbukwa kuwa mara ya mwisho Arsenal ilitwaa
taji la FA mwaka 2005 kabla ya jana usiku kuandika historia nyingine ya
kutwaa kombe hilo kwa mara ya tano.
“Siku zote nimekuwa nikisisitiza, kombe haliwezi kuwa kipimo
kwangu kama naondoka au nabaki. “Lakini nimekuwa nasisitiza kuwa nataka
kubaki Arsenal, hili si jambo geni hata kidogo. Alisema Wenger
Kama hukupata nafasi ya kutazama mchezo kati ya Arsenal na Hull City, itazame video hapo chini ya magoli .
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269