Naibu Katibu Mkuu akizungumza na Ugeni Kutoka chama rafiki cha National Resistence Movement(NRM)Kutoka Uganda waliofika Kujifunza Mambo mbalimbali ya Kiuongozi/Kiutendaji ndani ya Chama cha Mapinduzi.Naibu katibu Mkuu CCM-Bara, Mwigulu akimkabidhi Kitabu/cha Mwongozo cha Chama cha Mapinduzi Kiongozi wa Serikali ya Uganda(NRM).Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara, Mwigulu Nchemba akimkabidhi Katiba Ndugu Nnsiima Emmanuel Bigirwa Mchambuzi wa Mambo ya Siasa Kutoka Serikali ya Uganda.Mwigulu akimkabidhi kanuni za Uchaguzi zinazotumiwa na Chama cha Mapinduzi.
Ujumbe huu Kutoka NRM Wakifurahia Jambo kutoka Chama Cha Mapinduzi.Viongozi hawa Kutoka Uganda Wamefurahia sana Kupata Elimu ya namna Chama cha Mapinduzi kinavyojiendesha,Ikumbukwe Uganda kwa Muda mrefu imekuwa Ikiendesha siasa zake katika Mfumo wa Chama Kimoja,Ujio wa Vyama Vya Upinzani umekuwa Changamoto kwa chama cha NRM hivyo wanatumia fursa mbalimbali Kujifunza namna ya Kufanya siasa za Ushindani kama CCM inavyofanya hapa Tanzania.Upande wa Kulia ni Hon. Nabulya Ssentongo Theopista.Mwigulu Nchemba akipokea Zawadi Kutoka Ujumbe wa Chama cha NRM-Uganda.Mwigulu Nchemba akitoa Maelezo namna Chama cha Mapinduzi kinavyofanya Kazi zake na Muundo wa Uongozi Kuanzia Ngazi ya Shina hadi Tawi na Mfumo Mzima wa Uchaguzi unavyoendeshwa ndani ya Chama cha Mapinduzi.
Hafla hii imefungua Mlango Mkubwa zaidi wa Urafiki na Umoja kati ya Chama cha Mapinduzi na Chama Kinachoongoza Serikali ya Uganda cha National Resistence Movement Kutokana na Kuwekeana Malengo ya Kuendelea Kushirikiana Katika Uga wa Siasa na Nyanja zingine za Kiuchumi na Kijamii.
Picha/Maelezo na Sanga Jr
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269