Na Mwandishi,New York
Siku chache baada ya Bw. Lakhdar Brahimi ,Mjumbe wa Maalum wa Katibu
Mkuu na Muungano wa Nchi za Kiarabu
kujiuzulu na usulushi wa mgogo wa Syria. Wananchi wa Syria wamepata pigo jingine, baada
ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa
Mataifa, kushindwa kupitisha Azimio ambalo
lingeipeleka Syria katika
Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (
ICC).
Baraza Kuu la Usalama,
lilikutana siku ya alhamisi ili
kupigia kura rasimu ya Azimio
hilo lilowasilishwa na Ufaransa,
lakini likashindwa kupita baada ya Urusi na Uchina kupiga kura ya tururfu kupiga azimio hilo.
Wajumbe kumi na tatu kati ya 15 wanaounda
Baraza hilo, walipiga kura ya
kuunga mkono rasimu hiyo.
Kama Azimio hilo lingepita bila ya kupingwa, basi
ICC ingepewa dhamana ya kuchunguza makosa yote ya jinai na uhalifu wa kivita
kuanzia mwaka 2011 ulipoanza mgogoro wa
wenyewe kwa wenyewe ambapo zaidi ya watu 100.000 wamepoteza maisha huku
mamilioni wakiwa ni wakimbizi.
Katibu Mkuu Ban ki
Moon katika salamu zake zilizosomwa kwa niaba yake na Naibu Wake Bw. Jan Eliason, muda mfupi kabla ya
kupinga kura, amesema, Baraza Kuu la
Usalama na lile la haki za Binadamu
yanawajibika kumaliza umwagaji damu na kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwa
wahanga wa machafuko hayo.
Akaongeza kuwa
wananchi wa Syria wanayo haki ya msingi ya kupata haki. Umoja wa Mataifa na wananchama wake
wanaowajibu wakuilinda haki hiyo. Kwa kuunga mkono mifumo ambayo itawawajibisha
wahalifu wa makosa ya kivita. Na kusisitiza kwamba ni wazi
kuwa hakuna upande wowote kati ya zinazopingana ambao hauna kosa.
Akasisitiza kuwa kama
wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama wataendelea kuto kukubaliana kuhusu
njia zinazoweza kuleta uwajibikaji juu ya uhalifu unaoendelea,
hadhi ya chombo hicho muhimu na Umoja wa
Mataifa kwa ujumla itaendelea kuathirika.
“ Tunapozungumzia
uwajibikaji, lazima tufikirie si tu kwa pande zinazopingana, bali pia ni lazima
tuwafikirie na wale ambao wanaendelea kuchochea mgogoro huu na kuendelea kwa
madhara yanayotokana na wao kuendelea kutoa silaha kwa wale wanaotenda uhalifu” akasema Ban ki Moon.
Akawasihi wajumbe wa
Baraza Kuu la Usalama, kuweka pembeni tofauti zao na
kufanya kazi pamoja ili kuumaliza mgogoro wa Syria pamoja na kutafuta suluhisho
la kisiasa.
Kabla ya kuwasilisha wa Azimio hilo mbele ya Baraza Kuu la Usalama,
kulikuwa na taarifa za kidiplomasia kuwa waandaji wa Azimio hilo walikuwa wakiziomba nchi ambazo
si wajumbe wa Baraza Kuu kuunga mkono hali ambayo si ya kawaida.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269