Kampuni ya Clouds Media International leo imetangaza kuwa imepewa leseni ya kurusha matangazo katika nchi za umoja wa falme za kiarabu (UAE). Akielezea kuhusu leseni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bwana Joseph Kusaga (Pichani), amesema sasa kituo cha Clouds TV kimataifa kitakuwa kikishuhudiwa na watu wa mataifa mbalimbali.
Clouds TV kimataifa ni mwendelezo wa televisheni maarufu sana kwa
vijana nchini Tanzania, hata hivyo sehemu kubwa ya maudhui
yatakayokuwemo kwenye Clouds TV kimataifa itakuwa na mpangilio mpana wa vipindi
kwa watazamaji vitakavyorushwa kwa lugha
za Kiingereza na Kifaransa. Akieleza zaidi Kusaga amesema "Leo
ni siku ya kihistoria na alama ya hatua
moja katika mpango wetu wa kina wa kupeleka maudhui ya Clouds TV kimataifa
kupitia matangazo kwa njia ya mitandao’’.
Clouds TV kimataifa haitotoa tu burudani,
lakini pia itakuwa kiunganishi kwa waafrika waishio katika umoja wa nchi za
falme za kiarabu pamoja na kuwapa fursa za kutangaza bidhaa zao na kuimarisha uhusiano
baina yao.
Vituo vya televisheni katika Umoja wa falme za kiarabu vipo vingi na vyenye
ushindani mkubwa, lakini Clouds TV kimataifa imebahatika kupata nafasi ya
kurusha matangazo yatakayowafikia walengwa katika chaneli yenye uwezo wa
kuwahudumia zaidi ya watazamaji
takribani milioni 3.5 kutoka katika nchi za Afrika. Kwa sasa hakuna
kituo kinachotoa huduma hii na hivyo kuwa fursa muhimu kwa watazamaji.
Clouds TV kimataifa itarusha vipindi vya burudani, tamthilia, maigizo,
ucheshi, na muziki, vyote vitakavyo kuwa vimeandaliwa kutoka nchi za mashariki,
magharibi na kusini mwa bara la afrika na itapatikana
kwa watazamaji walio katika Umoja wa falme za kiarabu kupitia huduma ya IPTV inayotolewa na Etisalat na Du.
Clouds TV kimataifa itarushwa
kupitia mamlaka ya Abu Dhabi ijulikanayo kama twofour54, ikiungana na vituo
kama FOX na CNN. Clouds TV kimataifa
itaanza kurusha matangazo ya majaribio
katika wiki chache zijazo kabla ya tarehe 15 mwezi June mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269