Kamati za Uongozi wa kampuni ya Pan Africa Power (PAP) ambao ni wamiliki wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania ltd (IPTL) wamesema wameshangazwa na taarifa zilizochapisha na gazeti la Mtanzania la Toleo namba 7451 la jumatatu ya 05-05 2014 yenye kichwa cha habari kinachosema “KASHFA MZITO KAMATI ZA BUNGE” akizungumza na blog hii Mshauri na mwanasheria wa kampuni hiyo ya IPTL ,Joseph Makandege alisema wao kama kampuni wamechukulia taarifa iliyochapishwa na gazeti hilo kama Uchochezi na udhalilishaji mkubwa kwa kamati za bunge ya Nishat na Madini.
Akifafanua zaidi Mkandege alisema Kamati hiyo ya bunge walikutanao katika ofisi ndogo za bunge mara mbili na baadae kamati hiyo walipanga kutembelea Mitambo iliyopo Tegeta na siku ya waliotembelea mitambo hiyo kamati iliwastukiza wakati uongozi wa juu wa kampuni hiyo ulikua safarini lakini walipokelewa na plant meneja ambaye aliwatembeza wabunge hao na taarifa kuwasilishwa kwa viongozi baada ya kurejea sasa huyo mtu aliyewapokwea hana mamlaka yoyote kifedha kuweza kuipatia kamati hiyo alihoji Mkandege.
Akiongeza alidai wao kama kampuni wanachukulia kama changamoto tuu na mbinu chafu za wapinzani wao kibiashara akitolea mfano kwa sasa wao wana uza Unit moja shilling 26-30 tofauti na wapinzani wao kibiashara.
Alisema wao wana mpango wa kupunguza bei ya umeme mpaka kufikia senti 6-7 kwa unity endapo serikali itawauzia gesi kwa centy 3 kama walivyoahidi.
Alielezea sababu za wao kuuza unity kwa bei ya chini hivi sasa kuliko wapinzani wao kuwa ni kwasababu wanatumia malighafi ya mafuta mazito Have Fuel Oil na wapo kwenye mchakato wa kubadilisha mashine ili kutoa nafuu zaidi kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269