Breaking News

Your Ad Spot

May 7, 2014

DCB BENKI YATOA RIPOTI YA FEDHA YA MWAKA 2013-2014


Mkurugeni wa Benki ya DCB, Edmund Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya hesabu za mwaka uliopita. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Paul Rupia
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Paul Rupia akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya hesabu za mwaka uliopita. Kushoto ni Mkurugeni wa Benki ya DCB, Edmund Mkwawa

Na Mwandish wetu
Benki ya Biashara ya DCB inatarajia kufanya mkutano mkuu wa mwaka tareh 24 mwezi mei katika ukumbi wa Diamond Jubilee  jijini Dar es
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaamu jana Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Balozi Paul  Rupia,wakati akitoa matokeo ya hesabu za mwaka a 2013-2014.
Aliongeza kuwa katika  uendeshaji wa benki  lengo la amana lilifikiwa kwa kupata  shilingi bilioni 108 ikiwa ni ongezeko la asilimia 16 kutoka shilingi bilioni 90 zilizopatikana mwaka jana.
 Balozi Rupia alisema” mikopo katika benki yetu imeongezeka kwa asilimia 16 kutoka shilingi bilioni 67 mwaka jana hadi shilingi bilioni 78  mwaka 2013”. Alisema
Kwa Mujibu wa Rupia ongezeko la mikopo hiyo iliwanufaisha wajasiriamali walijiunga katika vikundi waishio Jijini Dar esSalaam na wafanyabiashara wadogo katika manispaa zote tatu jijini humo.
Rupia aliongeza kuwa Benki yao  iko  mstari mbele kuitumikia jamii  kwa kipindi cha mwaka 2013 ilishiriki katika sekta ya afya kwa kutoa mashine za Kupulia zenye thamani ya shilingi milioni 12.8 kwa hospitali za Temeke,Mwananyamala na Kinondoni za jijini Dar esSalaam.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Benki hiyo Edmund Mkwawa alisema “Benki yetu mwaka jana imepata faida mara mbili zaidi mwaka 2012, hii imetokana na benki hii kuwa na idara mbalimbali na huduma zinazovutia wateja wetu alisema
Huduma za benki kwa njia ya mtandao wa intaneti DCB Connect, DBC  Mobile na DCB jirani ambapo huanganisha wateja wa benki hiyo kupitia duka la jirani lenye nembo la DCB Jirani ambapo mwenye duka ni wakala wa benki. Alisema Mkwawa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages