Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa Msange,kata ya Msange,Singida
Vijijini mkoani Singida. Ndugu Kinana
akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape
Nnauye,leo wanahitimisha siku nane za ziara yao ya Kukagua kuhimiza na
kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa
kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za
mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.Kinana na
Msafara wake kesho unaelekea mkoani Manyara ambako ataendeleza ziara
yake.
Katibu
wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia Wananchi kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Msange,kata ya
Msange,Singida Vijijini mkoani Singida jioni ya leo.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimdondoshea tone la chanjo ya Polio mtoto
Erick Gabriel alipokwenda kukagua mradi wa Zahanati mpya ya
Mkenge,Singida Vijini mkoani Singida jioni ya leo.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (wa tatu Pichani) akishiriki kuvuna Mtama
katika shamba la Bwa.Khamis katika kijiji cha Mkenge,Singida Vijijini
akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini ,ambaye pia
Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh.Lazaro Nyalandu.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupembua Mtama kwa njia ya
mashine,ambayo ndiyo njia ya kisasa inayoweza kurahisha kazi kwa
mkulima,mashine hiyo ina uwezo wa kupembua magunia sita mpaka kumi kwa
saa.kulia kwake ni Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi Nape Nnauye
akishuhudia.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa sambamba na Mbunge wa Jimbo la Singida
Kaskazini,Mh.Lazaro Nyalandu wakishiriki ujenzi katika Kiwanda cha
kusindika na kusafisha mafuta ya Alizeti,katika kijiji cha
Mtinko,Singida Vijijini mkoani Singida jioni ya leo
Kinana
akitoka kukagua mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha kusindika na kusafisha
mafuta ya Alizeti,katika kijiji cha Mtinko,Singida Vijijini mkoani
Singida jioni ya leo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269