Breaking News

Your Ad Spot

May 10, 2014

KINANA AFUNGA KAZI IGUNGA, APIGA KAZI ZA NGUVU, MAELFU WAHUDHURIA MKUTANO WAKE WA HADHARA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga leo, Mei 9, 2014, akiwa katika ziara ya siku kumi kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua na pia kuimarisha uhai wa chama mkoani Tabora
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape NNauye akizungumza kwenye mkutano huo
Maelfu ya wananchi wakinyoosha mikono kumshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara Mei 9, 2014, kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga
Mkuu wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora Elibariki Kingu, akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM kwenye mkutano huo wa Kinana auliofanyika, Mei 9, 2014 kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine wilayani humo.

Kinana akirudi hotelini kwa miguu baada ya mkutano, pembeni yake ni Nape

KUIMARISHA UHAI WA CHAMA
Kinana akizindua Ofisi ya CCM tawi la Igogo, Kata ya Nanga Igunga, mkoani Tabora, leo Mei 9, 2014
 Kinana akizungumza baada ya kuzindua Ofisi hiyo ya CCM tawi la Igogo, Kata ya Nanga Igunga. Kulia ni Nape
Kinana akisalimia baadhi ya wazee baada ya kuzindua tawi hilo la CCM
Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya msingi Mihama, Igunga mkoani Tabora, Mei 9, 2014. Kushoto ni DC Igunga, Elibariki Kingu akisaidia kubeba tofali kumpa Katibu Mkuu Kinana.
 Kinana akiwa na bango lenye ujumbe maridhawa, kumkaribisha Kinana, alipotembelea shamba la alizeti la Vijana wajasiriamali, eneo la Iborogero, wilayani Igunga mkoani Tabora, Mei 9, 2014, ikiwa ni sehemu ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika muktadha wa ajira kwa vijana.
 Kinana akikagua shamba hilo la alizeti la Vijana la Iborogelo
 Kinana akitazama zao la alizeti alipokagua shamba hilo la alizeti la Vijana la Iborogelo
 HADI KULEEEE KOTE NI SHAMBA LETU: Kinana akimwambia Kinana wakati akimuonyesha shamba hilo la alizeti ambalo limesaidia vijana wa kada mbalimbali kujiajiri
 Katibu Mkuu, Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na vijana wanaoshiriki mradi huo wa kilimo cha alizeti, Iborogero wilayani Igunga mkoani Tabora.
 Mwenyekiti wa Vijana SACCOS ya Igunga, Frey Cosseny (wapili kushoto) akiwatambulisha kwa Kinana maofisa wengine wa SACCOS hiyo, Mei 9, 2014 alipofika kukagua shuguli za SACCOS hiyo na kuzungumza na wanachama.
 Katibu Mkuu Kinana akiwasalimia wadau wa SACCOS hiyo
 Kinana akiendesha trekta la mradi wa Igunga Vijana Saccos kulizindua
 Kinana akishuka kwenye trekta baada ya kulizindua la Vijana SACCOS ya Igunga
Katibu Mkuu Kinana akikabidhi funguo kwa mmoja wa Wana-SACCOS hiyo, Joseph Kashindye, wakati alipokagua shughuli za SACCOS hiyo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika mkoa wa Tabora, Mei 9, 2014. (Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages