Breaking News

Your Ad Spot

May 13, 2014

KINANA AKAGUA UJENZI NYUMBA ZA WATUMISHI,KITUO CHA POLISI NA JENGO LA HALMASHAURI MAKAO MAKUU YA WILAYA YA UYUI,TABORA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Ufuluma, Jimbo la Tabora, wilayani Uyui, ambapo alizungumzia jinsi serikali  ilivyoazimia kuboresha sekta ya maji umeme na elimu vijijini.

 Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Ufuluma ambapo waliwafananisha wapinzania na fisi aliyejifanya ana pembe kwenye mkutano wa wanyama wenye pembe.

 Kinana akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, mkoani Tabora, ambapo alikagua ujenzi wa nyumba 8 za watumishi ,  Hospitali ya Wilaya, Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo, Kituo cha Polisi na Jengo la Kituo cha Polisi.

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Lucy Mayenga wakati Kinana alipotembelea Makao Makuu ya wilaya hiyo eneo la Isikizya.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wakimsikiliza Kinana alipowatembelea leo

 Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Ujenzi Wilaya ya Uyui, Steven Nyanda kuhusu ujenzi wa nyumba za watumishi wa wilaya hiyo.

 Moja ya nyumba za za watumishi wa wilaya ya Uyui zilizojengwa kwa mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.

 Kinana akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Uyui eneo la Isikizya

 Kinana aakikagua ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya Uyui

 Kinana akielekea kukagua chanzo cha maji katika eneo la Isikizya

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa akielezea jinsi alivyofanya jitihada za kuuendeleza makao makao makuu ya wilaya ya Uyui.

 Kinana na Nape wakikagua ujenzi wa nyumba 50 za watumishi

 Kinana, Nape wakipanda miti katika eneo la Shule ya Sekondari ya Ilolangulu wilayani Uyui

Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Lucy Mayenga akitoa taarifa ya utekelezaji wa  Ilani ya CCM katika wilaya hiyo

Kinana akizhutubia katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Uyui ambapo alisomewa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM

Mwalimu wa somo la kemia wa Shule ya Sekondaro Ndono, wilayani Uyui, Mahubira Chandarawa akimuonesha Kinana jinsi ya kutumia vifaa vya maabara alipokagua maabara ya shule hiyo ya Kata.

Nape  9mbele0 akikagua jengo la maabara la Shule ya Sekondari ya Ndono, wilayani Uyui.

Kinana akikagua jengo la Zahanati ya Kata ya Ufuluma, Tabora Kaskazini, wilayani Uyui

Kinana akiwasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Ufuluma, wakati wa ziara yake wilayani Uyui.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Tabora, Mwanne Nchemba, akihtubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Ufuluma.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Ufuluma ambapo azingumzia matatizo yanayowakabili wakuliama wa zao la tumbaku.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, akizungumza katika mkutano huo wa hadhara na kuelezea jitihada zinazofanywa kuboresha sekta ya afya, elimu, maji na barabara wilayani humo.

Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini, Shaffin Sumar na Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Lucy Mayenga wakisikiliza kwa makini wakati Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano huo.

Kinana akiwa na Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Uyui, ambaye alimtaka kuelezea mipango ya ujenzi wa visima saba katika Kata ya Ufuluma.

Baadhi ya wana CCM wakila kiapo cha utii cha chama hicho  katika mkutano huo

Baadhi ya walimu wa wilaya za Uyui na Tabora Mjini wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM, alipokuwa akizungumza nao kuhusu matatizo mbalimbali yanayowakabili na jinsi ya kuyasuluhisha.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  akizungumza na waalimu wa shule katika Wilaya za Uyui na Tabora Mjini, jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo kukatwa sehemu ya mishahara yao, kunyimwa fedha za zikizo,  ukiritimba wa kupandishwa vyeo na mengineyo. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages