Breaking News

Your Ad Spot

May 26, 2014

MWENGE WA UHURU 2014 WAMALIZA MBIO ZAKE MKOANI RUKWA LEO, WAMMULIKA MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) ALIYEKATWA MKONO MWAKA JANA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (katikati) akishiriki mbio za Mwenge wa Uhuru (2014) na viongozi wa mbio hizo kitaifa, viongozi na wafanyakazi wa Serikali, vyama vya siasa Mkoani Rukwa na wananchi muda mfupi kabla ya kukabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro baada ya Mwenge huo kukamilisha mbio zake Mkoani Rukwa leo tarehe 25-05-2014. Mwenge huo wa Uhuru mkoani Rukwa ulitembelea miradi ya maendeleo 28 na vikundi 27 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni nne (4). 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro Mwenge wa Uhuru baada ya kumaliza mbio zake Mkoani Rukwa leo tarehe 25-05-2014. Mwenge huo wa Uhuru mkoani Rukwa ulitembelea miradi ya maendeleo 28 na vikundi 27 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni nne (4). 
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru (2014) kitaifa Ndugu Wito Mlemelwa (katikati) kwa niaba ya Kiongozi wa wakimbiza Mwenge kitaifa (2014) Ndugu Rachel Kassanda akimkabidhi mlemavu wa ngozi Bi. Maria Chambanenge mkazi wa Sumbawanga msaada wa ng'ombe wawili wa kulimia aina ya Maksai (hawapo pichani) na jembe la kulimia wanyama (Plau) jana tarehe 24-05-2014 vikiwa na thamani ya Tsh. Milioni 2.3 kama msaada wa kujikimu kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kutokana na mama huyo kukatwa mkono wake wa kushoto kwa imani za kishirikina mwishoni mwa mwaka jana. Kushoto anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Methew Sedoyyeka.
Ng'ombe wawili wa kulimia aina ya Maksai waliotolewa msaada kwa Mama Maria Chambanenge.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru (2014) kitaifa Ndugu Wito Mlemelwa (katikati) kwa niaba ya Kiongozi wa wakimbiza Mwenge kitaifa (2014) Ndugu Rachel Kassanda akimkabidhi mlemavu wa ngozi Bi. Maria Chambanenge mkazi wa Sumbawanga msaada wa jembe la kulimia wanyama (Plau) na ng'ombe wawili wa kulimia aina ya Maksai (hawapo pichani) jana tarehe 24-05-2014 vikiwa na thamani ya Tsh. Milioni 2.3 kama msaada wa kujikimu kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kutokana na mama huyo kukatwa mkono wake wa kushoto kwa imani za kishirikina mwishoni mwa mwaka jana. 
Mlemavu wa ngozi Bi. Maria Chambanenge mkazi wa Sumbawanga ambaye alisababishiwa ulemavu mwingine wa viungo mwaka jana 2013 na watu wasiojulikana baada ya kukatwa mkono wake wa kushoto kwa imani za kishirikina akishika Mwenge wa Uhuru jana tarehe 24-05-2014 ulipotembelea kijijini kwao kuzindua mradi wa maji na kumkabidhi msaada wa ng'ombe wawili wa kulimia aina ya Maksai (hawapo pichani) na jembe la kulimia wanyama (Plau) vikiwa na thamani ya Tsh. Milioni 2.3 kama msaada wa kujikimu kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa mama huyo. 
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages