Breaking News

Your Ad Spot

May 26, 2014

RAIS WA KLABU YA BONGO MOVIE STEVE NYERERE AKABIDHI JEZI NA MIPIRA SITA KWA VIJANA WA KINONDONI


Rais wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steve Mengere "Steve Nyerere" katikati akiwakabidhi vijana wa Kinondoni Jezi na mipira sita Ikiwa nisehemu yake ya kujitoa Kwa Jamii kwa kile alichoweza. Steve alisema kuwa yeye ameweza kutoa kile kidogo alichoweza kuwa nacho na anaamini kuwa Jezi pamoja na Mipira hiyo Sita itaweza kusaidia kuamsha hali ya michezo kwa Vijana Hao Wa Kinondoni na kuhaidi pia ataendelea kuwasaidia vijana wa kitanzania katika michezo pale anapoweza kufanya hivyo. Vijana wa Kinondoni Wamshukuru pia Kwa kuweza kutoa hata hiko kidogo kwani wanaamini kutoa ni Moyo na Sio Utajiri.
 Kiongozi wa Vijana wa Kinondoni akipokea Jezi kwa Niaba ya Wenzake kutoka kwa Rais wa Bongo Movie Unity Steve Nyerere mwishoni mwa wiki
 Wakiwa katika Picha ya Pamoja mara baada ya kuwakabidhi Jez na Mipira Sita.

Mwishoni mwa Wiki Rais wa Bongo Movie Unity, Steve Mengere, "Steve Nyerere" aliwakabidhi vijana wa Kinondoni Jumla ya Mipira 6 na jozi moja ya Jezi za mpira wa miguu ikiwa ni sehemu ya kujitoa kwake kwa Jamii iliyomzunguka.

Steve alisema kuwa ameweza kutoa kile kidogo alichonacho kwaajili ya kuinua hali ya michezo kwa vijana hao wa Kinondoni kitu ambacho anaamini kuwa vijana hao watapa hali ya michezo na kuachana na vitendo viovu katika Jamii, Vilevile aliongezea kusema kuwa ataendelea na moyo huyo kwa kutoa japo kile kidogo atakachopata kwaajili ya kuendelea kuwasaidia vijana wa Kitanzania katika Nyanja mbalimbali kwa kuanza ameanza na vifaa vya michezo kwa vijana hao wa Kinondoni.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages