Breaking News

Your Ad Spot

May 26, 2014

REAL MADRID YATWAA UBINGWA WA ULAYA, YAITANDIKA BAO 4 -1 ATLETICO


Diego Godin
Mchezaji wa Atletico Madrid, Diego Godin akishangilia baada ya kupachika goli la kwanza

Kikosi cha Real Madrid kinachonolewa
na Kocha Carlo Anceloti hatimaye kimeweza kutwaa ubingwa wa ligi ya
mabingwa barani Ulaya kwa mara ya kumi baada ya kuipa kipigo cha jumla
ya  bao 4 – 1 timu ya Atletico Madrid katika mtanage uliochezwa katika 
dimba la Estádio do Sport Lisboa nchini Ureno.

Atletico ndio waliokuwa wa kwanza
kuzifumania nyavu za Madrid kupitia mchezaji wake ‘Diego Godin’ mnamo
dakika ya 36′ kabla ya kusawazishwa na Sergio Ramos dakika za nyongeza
kipindi cha pili cha mchezo na kufanya matokeo kuwa suluhu ya moja moja.

Hata hivyo kibao kiliwageukia
mabingwa hao wa Hispania katika kipindi cha dakika 30′ za nyongeza, 
baada kuruhusu  magoli matatu yaliyoipa tiketi ya ushindi Madrid huku
yakifungwa na Gareth Bale DK ya 110′, Marcelo DK ya 118′ pamoja na
mkwaju wa penalti uliopigwa na Straika Mreno ‘Cristiano Ronaldo’ baada
ya kuangushwa.

Mashabiki wa Ral MadridMashabiki wa klabu ya Real Madrid wakiwa kwenye majonzi kabla ya timu yao kusawazisha.

Sergio Ramos
BEKI
tegemezi wa Real Madrid, Sergio Ramos akishangilia kwa staili ya aina
yake baada ya kusawazisha bao dakika za majeruhi za kipindi cha pili cha
mchezo



Gareth Bale
STRAIKA wa Real, Gareth Bale akishangilia baada ya kupachika bao la Tatu

Cristiano RonaldoCristiano Ronaldo akifanya yake

Zidane na Carlo Anceloti

Madrid Mabingwa wa UEFA Iker Casillas

Wachezaji wa madrid wakiongozwa na kipa wa timu hiyo Iker Casillas aliyeshika kombe wakishangilia kunyakua ubingwa wa UEFA

Tazama Video za Magoli hapo chini…
https://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=z-7tHcVswgM#t=0
https://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=OlvTelZ-4oM#t=0

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages