Meneja wa Wakala wa
huduma za Misitu Tanzania (TFS) kanda ya kaskazini Bw. Cuthbert Mafupa
akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) waliotembelea hifadhi ya Chome
kujionea hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kutunza misitu pamoja na
mafanikio yaliyofikiwa katika utunzaji wa hifadhi ya msitu wa Mazingira
asilia wa chome (Shengena) ikiwemo kupanda miti katika maeneo yaliyoathika na
uvunaji haramu wa rasilimali za msitu huo.
|
Prof.
Vicky Mckinley ambaye ni Mtafiti kutoka chuo Kikuu cha Roosevelt kilichopo
Chicago,Illinois nchini Marekani akipongeza juhudi za Serikali ya
Tanzania katika kutunza hifadhi ya Msitu wa mazingira asilia wa Amani uliopo
Wilayani Muheza Mkoani Tanga,wakati wa ziara ya Waandishi wa habari katika
Msitu huo hivi karibuni.
|
Msaidizi
wa Misitu Mkuu ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Zigi katika hifadhi ya Msitu wa
asili Amani bw. Mlega Sossele akiwaeleza waandishi wa habari hawapo
pichani jinsi wananchi wanavyonufaika na Msitu huo kwa kuwatengea asilimia 20
ya mapato yanayopatikana kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
|
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269