Muonekano wa Jengo jipya la Taasisi ya
Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI) ambalo linatarajiwa
kukamilika mapema mwaka huu,kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia Taasisi hiyo
kupanua huduma zake na kupunguza idadi ya wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje ya
nchi kwa kwa asilimia 80 ikiwa ni juhudi za Serikali kuboresha huduma za Afya
hapa nchini.
Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI) Bw. Jumaa
Almasi (katikati)akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatua
iliyofikiwa katika kupanua huduma za Taasisi hiyo ikiwemo kukamilika kwa
jengo jipya la kisasa litakalokuwa na vifaa vya kisasa kama MRI ( magnetic
Resonance Imaging) CT-SCAN (Computerized Tomography).kushoto ni Afisa Habari
wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum na kulia ni Afisa uhusiano wa
Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi.Picha zote na Idara ya
Habari Maelezo
---
Dar es Salaam,
26/05/2014 Mradi wa jengo jipya la MOI, (MOI Phase III) ambao utagharimu zaidi
ya Tshs billion 30 utaisaidia serikali kupunguza gharama za rufaa za kuwapeleka
wagonjwa nje ya nchi kufuata huduma kutokana na
baadhi ya huduma na vipimo kutokuwepo nchini,rufaa hizo huwa ni za gharama kubwa sana.
|
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269