“PRESS RELEASE” TAREHE 24.05.2014.
- MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA JIWE KICHWANI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUKUTWA NA BHANGI.
TUKIO LA KWANZA.
MTU
MMOJA BARIKO MWAKASISILE [40], MKAZI WA KIJIJI CHA NYELELE- BUJONDE
WILAYA YA KYELA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU
KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA TAREHE 23.05.2014 MAJIRA YA SAA
16:00HRS ALASIRI.
MAREHEMU
ALIPIGWA JIWE KICHWANI NA LUPAKISYO JACOB, MKAZI WA KIJIJI HICHO.
TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 19.05.2014 MAJIRA YA SAA 23:00HRS USIKU
HUKO KATIKA KITONGOJI CHA NYELELE, KIJIJI NA KATA YA BUJONDE TARAFA
YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA. CHANZO CHA TUKIO HILO KINACHUNGUZWA NA
MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI
ALIPOKIMBILIA MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
KATIKA MSAKO.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI [02] KUTOKANA NA
MISAKO MBALIMBALI ILIYOFANYIKA. KATIKA TUKIO LA KWANZA JESHI LA
POLISI LINAMSHIKILIA MTU MMOJA THOMAS BENEDICTO [30], MKAZI WA MBUGANI
– KYELA KWA KUKUTWA NA BHANGI KETE 62 ZENYE UZITO WA GRAMU 460 PAMOJA
NA BHANGI AMBAYO BADO HAIJASOKOTWA GRAM 500,YOTE IKIWA NA UZITO WA GRAM
960.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 23.05.2014 MAJIRA YA SAA 08:30HRS ASUBUHI HUKO
ENEO LA KALUMBULU, KATA YA KYELA – KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA.
MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI, TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA
TUKIO LA PILI JESHI LA POLISI LIMEMKAMATA MTU MMOJA MWANGOTA
MWANGOTA [40], MKAZI WA KIJIJI CHA IBUNGU KYELA KWA KUKUTWA NA BHANGI
KETE 70 ZENYE UZITO WA GRAMU 350.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 23.05.2014 MAJIRA YA SAA 09:45HRS ASUBUHI HUKO
ENEO LA MBUGANI, KATA YA KYELA KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA. MTUHUMIWA NI
MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA
DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI.
Imesainiwa na
[ B.N.MASAKI – ACP ].
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269