Premi Kibanga,-Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
--
“Nimepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Bwana Maximilian kilichotokana na
maradhi ya Moyo, Sukari na Shinikizo la
damu. Kifo hicho ni pigo na pengo kubwa kwa tasnia ya habari hapa nchini,”Amesema
Rais Kikwete katika salamu hizo.
“Bw. Maximilian
atakumbukwa kwa uchapakazi wake na uhodori katika kazi zake siku zote. Kifo ni
maandiko ya Mwenyezi Mungu hivyo hatuna budi kumshukuru kwa yote.
“Nakutumia salamu zangu
za dhati kuomboleza msiba huu. Aidha, kupitia kwako, naitumia familia ya Ndugu
Maximilian, pole za dhati ya moyo wangu kwa kuondokewa na mzazi na mhimili wa
familia. Aidha, salamu hizi ziwafikie pia wanahabari wote, wafanyakazi wenzake,
ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu. Nakuomba uwajulishe kuwa naelewa machungu
yao katika kipindi hiki na nawaombea subira na uvumilivu. Ninaungana nao
kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa
Rehema, aiweke peponi roho ya marehemu. Amen,” amesema Rais katika salamu hizo.
Ndugu Maximilian John
ameacha mke na watoto wanne.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
24 Mei,2014
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269