TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Kufutia
kuibuka kwa vikundi vya vijana vinavyojulikana kwa majina ya mbwa
mwitu, watoto wa mbwa au Panya road na kujihusisha na vitendo vya
kihalifu ikiwemo uporaji, unyang’anyi wa kutumia nguvu na kujeruhi watu
katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam, Naibu Inspekta Jenerali
wa Polisi (DIGP) Abdulrahaman Kaniki amewaagiza makamanda hususani wa
Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuhakikisha wanavitafuta vikundi hivyo
popote vilipo, kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Naibu
IGP amekemea vikali vikundi hivyo na kuvitaka kuacha tabia hiyo mara
moja, kwani vitendo hivyo ni vya kihalifu na vinatakiwa kukemewa na kila
mtu katika jamii.
Aidha,
amewataka wananchi kuondoa hofu na badala yake watoe ushirikiano kwa
kutoa taarifa za vikundi hivyo katika vituo vya Polisi ili hatua za
haraka ziweze kuchukuliwa.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269