Breaking News

Your Ad Spot

May 24, 2014

Tangazo la Shukrani


Angela Novatus Matiku
30.09.1981 – 07.04.2014

Familia ya Brg. Gen mstaafu Novatus M. Matiku inatoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na majirani wote walioshirikiana nasi kwa hali na mali kipindi chote cha msiba wa binti yetu mpendwa Angela (Gaya) aliyetutoka ghafla tarehe 07 Aprili, 2014, na kuzikwa tarehe 11 Aprili, 2014.  Mmetupatia faraja kubwa sana katika kipindi hicho kigumu kwa familia.

Familia inatoa shukrani za dhati kwa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Andrea Mtume, Bahari Beach kwa kuendesha ibada ya kumuaga Angela nyumbani Bahari Beach, Parokia ya Mt.Yohana Mugango, Musoma kwa kuendesha ibada ya mazishi.

Kwa namna ya pekee, familia inatoa shukrani za dhati kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania Generali Davis A. Mwamunyange na familia yake; Wafanyakazi waliowahi kufanyakazi na Angela wa Camfed, NIMR Muhimbili, Vodacom Tanzania, Angela Catering Services na wengineo wote;  Marafiki wote wa karibu wa Angela; Madaktari wa Hospitali za Kinondoni, Regency na Muhimbili kitengo cha Emergency, Majirani wa Bahari Beach, Mwenge Kijijini na Lugalo; Jumuiya ya Mt. Dominic Bahari Beach; Wanajumuia na wanakwaya wa Kanisa katoliki la Mwenge; na umoja wa wanakijiji wa Mugango kwa huduma zote za hali na mali walizozitoa kipindi chote cha msiba.

Kwa vile si rahisi kuwataja wote, kwa taarifa hii tunawaomba mpokee shukrani zetu za dhati kwa moyo wa upendo mkubwa mliotuonyesha.
Misa ya Shukrani itafanyika siku ya Jumamosi 24 Mei, 2014 katika kanisa katoliki, Bahari Beach saa 1:00 asubuhi. Familia inapenda kuwakaribisha ndugu, jamaa na marafiki wote siku hiyo kanisani au nyumbani kuanzia saa 5 asubuhi kuwa pamoja na kumshukuru mungu na kusherehekea maisha ya Angela.

MUNGU AILAZE ROHO YA ANGELA MAHALI PEMA PEPONI APUMZIKE KWA AMANI, AMINA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages