Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Profesa Makame Mbarawa (katikati) na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Jenista Muhagama, wakimsilikiza Afisa Uhusiano wa Chuo cha Kikristo cha Uganda
Prim Tumuramye baada ya ufunguzi wa Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu, Sayansi na
Teknolojia yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Jenista Muhagama, akimueleza jambo Naibu Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Dar
es Salaam (DUCE) Profesa Godliving Mtui (katikati) kwenye ufunguzi wa Maonesho
ya 9 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa
Diamond Jubilee.Kulia ni Waziri wa Mawsiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa
Makame Mbarawa.
Mtaalamu wa Masuala ya Lishe kutoka Chuo
Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Gaudensia Donati akimueleza jambo Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Muhagama (anayeonekana mikono),wakati
walipotembelea banda la chuo hicho.
. Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, akiangalia aina za panya wanazalishwa na
Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) katika Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu,
Sayansi na Teknolojia yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, akimueleza jambo Makamu Mshauri wa Wanafunzi
wa Shule ya Kimataifa ya Elimu iliyoko chini ya Chuo Kikuu cha Syansi na
Teknolojia cha Huazhong cha nchini China, Annie Zhao wakati alipotembelea banda
la chuo hicho.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar,
Profesa Idris Rai akiwaonesha jambo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia Profesa Makame Mbarawa (katikati) na Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Jenista Muhagama, wakati walipotembelea banda la chuo hicho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269