Breaking News

Your Ad Spot

May 24, 2014

ZIARA YA KINANA WILAYA YA MKALAMA YAFANA LEO, AKAGUA UJENZI DARAJA LA SIBITI LINALOUNGANISHA SINGIDA NA SIMIYU AHUTUBIA MAMIA YA WANANCHI KATIKA MIKUTANO YA HADHARA

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone (aliyenyoosha mkono) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa daraja linalounganisha mikoa ya Singida na Simiyu katika  mto Sibiti, Kinana alipokagua ujenzi wa daraja hilo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadsiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya ya Iramba leo Mei 24, 2014. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye amefuatana na Kinana katika ziara hiyo. Ujenzi wa daraja hilo unaogharimu sh. bilioni 16, unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitazama nguzo ya daraja linalojengwa kuunganisha mikoa ya Singida na Simiyu katika  mto Sibiti, Kinana alipokagua ujenzi wa daraja hilo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadsiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya ya Iramba leo Mei 24, 2014
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman  Kinana akitoa orodha ya vijiji vitakavyopata huduma ya umeme katika wilaya ya Mkalama, alipohutubia mkutano wa hadharakwenye  kijiji cha Nkungi, Wilaya humo leo, Mei 24, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadsiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape, akihutubia kwenye mkutano huo wa Nkungi, wilayani Iramba
Nape akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba kuhutubia kwenye mkutano huo.
Mwigulu akihutubia katika mkutano huo wa  Nkungi, Wilaya ya Mkalama
Mbunge wa Iramba Mashariki Salome Mwambu akihutubia katika kijiji cha Nkungi, Wilaya ya Mkalama
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza na Naibu Kamanda wa UVCCM mteule wilaya ya  Mkalama, Alan Kiula baada ya kuzindua Ofisi ya CCM wilaya mpya ya Mkalama. Kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na wapili kulia ni Mbunge wa Vito Maalum, Martha Mlata
Kinana na Nape wakiondoka baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Nkungi, wilayani Ilamba. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages