Breaking News

Your Ad Spot

Jun 21, 2014

ADY BATISTA WA “THE THORN OF THE ROSE” AKONGA NYOYO ZA WAPENZI WA SINEMA TAMASHA LA ZIFF 2014

DSC_0128
ADY de Batista (30).
DSC_0154
ADY de Batista akisaidiwa kushuka kwenye gari na meneja wake Sholey Maqueta mara baada ya kuwasili kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

Na Mwandishi wetu, Zanzibar
ADY de Batista alishuka taratibu katika gari la Noah, akiwa amevalia nguo nyeupe.Alisaidiwa kushuka kwenye gari na meneja wake Sholey Maqueta na kuingia katika ukumbi wa maonesho ya sinema wa wazi uliopo Ngome 

Kongwe kwa ajili ya sinema yake ya O Espinho Da Rosa.
Kutoka kwenye gari hadi alipopokewa na Mtendaji wa tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (ZIFF) Profesa Martin Mhando,unamuona mdada anayejiamini, mwenye uzuri wa asili na weusi unaong'aa majira ya magharibi kabisa, kabla ya swala ya insha.
DSC_0157
ADY de Batista akiingia kwenye lango kuu la Ngome Kongwe.
Alikuwa anatembea taratibu kama malkia kushoto akiwawepo meneja Sholey na Kulia rafiki yake wa kiume Antoine Simonet.Nyuma alikuwapo mdogo wake Nautenle Batista.

Alipokewa na Mtendaji wa ZIFF Profesa Martin Mhando ambaye alizungumza kidogo kuhusu O Espinho Da Rosa (The Thorn Of The Rose) kabla ya kumkaribisha kuzungumza na wapenzi wa sinema waliokuwa wamejazana pomoni katika ukumbi wa sinema.
DSC_0181
ADY de Batista na Meneja wake wakielekea kwenye jukwaa la ZIFF 2014 kuhutubia. 

Kabla ya kuzungumza kuhusu filamu hiyo ambayo imechezwa na Júlio Mesquita, mwenyewe Ady Batista, Daniel Martinho, Ângelo Torres na Ciomara Morais, Ady alishukuru kuwepo Zanzibar na kusema kwamba ndoto yake imetimia, anashukuru sana.

Sinema hii ambayo ni saa moja na dakika 37, ni sinema yenye makali yote ya maisha, mashaka na pia imani zilizojikita vyema katika jamii ambayo imekuwa ikikabiliwa na matatizo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages