Breaking News

Your Ad Spot

Jun 22, 2014

VIONGOZI WA KAMATI ZA AFYA ZA SHEHIYA WAPATIWA MAFUNZO JUU YA MIKAKATI YA AFYA YA JAMII ZANZIBAR

Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hassan Mussa Takrima akitoa nasaha kwa washiri wa mafunzo ya siku tano juu ya mkakati wa Afya ya jamii kwa viongozi wa kamati za Afya za Shehiya, katika ukumbi wa Ofisi ya walemavu Kikwajuni weles Mjini Zanzibar.
 Afisa Mipango na Utumishi wa Wilaya ya Magharibi Unguja Bw. Ameir Ali Haji akitoa maelezo juu mafunzo ya siku tano kwa viongozi wa kamati za Afya za Shehiya tatu za Magharibi, (kulia) Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hassan Mussa Takrima ambae ni mgeni rasmin katika mafunzo hayo. Yaliofanyi ukumbi wa Ofisi ya walemavu Kikwajuni weles Mjini Zanzibar.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo.
 Muezeshaji kutoka kitengo cha elimu ya Afya ya jamii Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Amina Sleyum akitoa mafunzo juu ya elimu ya Afya kwa jamii.

 Washiriki wakifanya mtihani.
(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar). 


MKUU wa Wilaya wa Magharibi, Hassan Mussa Takrima amewataka watendaji wa wizara ya afya kushirikiana na masheha katika kuelimisha wananchi juu ya utekelezaji wa mpango wa afya kwa jamii ili uweze kutatua changamoto za kifya nchini.

Amesema kuwa endapo mpango huo ukihamasishwa kwa jamii utaweza kuwasaidia wananchi katika kujikwamua na matatizo ya kujikinga na maradhi mbalimbali yanayojitokeza katika maeneo yao .
Akizungungumza katika ufunguzi wa mafunzo juu ya mkakati wa afya ya jamii kwa kamati kiongozi  za shehia za Magogoni,Meli nne na Chukwani zilizopo katika wilaya Magharibi ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi katika kupunmguza matatizo ya kifya yanayozikabili shehia hizo.
Alieleza kuwa serikali ya mapinduzi Zanzibar imeamua kutoa fursa kwa watendaji wa sekta ya afya waweze kufanya kazi kwa mashirikiano na viongozi kuanzia ngazi ya shehia kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na afya bora.
“Tumieni mafunzo yenu vizuri kwa hekima na upole kwani nyinyi mnaenda kuielimisha jamii, na uko kuna makundi mbalimbali yanayotakiwa kupewa taaluma juu ya umuhimu wa kutunza afya na utekelezaji wa mpango huu kwa vitendo.”alisema Takrima.
Nae Afisa wa afya  wa wilaya hiyo, Abubakar Mohamed Ali ameeleza kuwa katika katika mafunzo hayo washiriki watafundishwa njia mbadala ya kuwawezesha masheha na viongozi wengine kutumia rasilimali zilizomo katika maeneo yao ili kutatua changamoto za kiafya bila kusubili utekelezaji kutoka  serikali kuu.
Kwa upande wake afisa mipango wa Wilaya hiyo Ameir Ali Haji alifamisha kuwa  lengo la mkakati huo ni kuimarisha mahusiano baina ya sekta ya afya na jamii ili kuinua huduma za afya zinazotolewa ziweze kuendana na viwango vilivyowekwa na serikali.
NA MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages