Breaking News

Your Ad Spot

Jun 21, 2014

Kampuni ya Strabag International inayojenga barabara ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart) imetangaza mabadiliko ya muda katika eneo la Ubungo mataa leo na kesho usiku kutokana na ujenzi unaoendelea wa barabara.

Ujenzi huo utasababisha kufungwa kwa baadhi ya njia katika barabara hizo kuanzia leo saa nne usiku hadi kesho saa 12 asubuhi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Yahya Mkumba alisema kazi hiyo itahusu ujenzi katika makutano ya Barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Nelson Mandela.
Katika awamu ya kwanza, ujenzi huo utahusisha eneo la upande wa kulia la makutano la Barabara ya Sam Nujoma na Morogoro ambalo litafungwa.
“Hali hii itasababisha magari yanayotoka maeneo ya Buguruni na Tabata kwenda Mwenge kutokutumia njia ya Sam Nujoma watakapofika taa za Ubungo,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages