Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Laurance
Kabigi akimuonesha kifaa cha kuzimia moto Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Mh. Mathias Chikawe wakati Waziri huyo alipotembelea Mabanda
ya Wizara yake jana katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea
katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam .
Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Mathew E. Ikomba akitoa
maelezo ya namna Idara hiyo ilivyofanikiwa kutumia teknolojia mpya
ya utoaji wa vibali vya ukaazi kwa mfumo wa kielectroniki na hivyo kuondokana
na mfumo wa awali wa kuandika vibali hivyo kwa mkono, mbele ya
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe wakati Waziri
huyo alipotembelea Mabanda ya Wizara yake jana katika Maonyesho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe
akipokea vijitabu vidogo vinavyoelezea masuala ya utendaji wa
polisi kutoka kwa afisa wa Jeshi la Polisi Christina Mponji wakati
Waziri huyo alipotembelea Mabanda ya Wizara yake jana katika Maonyesho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam .
Maafisa wa jeshi la Magereza wakifurahia jambo pamoja
na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe wakati
Waziri huyo alipotembelea Mabanda ya Wizara yakejana katika Maonyesho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari Mkuu na Msemaji wa Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa (NIDA) Thomas Willium wa kwanza kushoto akitoa maelezo
ya namna Mamlaka hiyo inavyotekeleza zoezi la kuandaa na kutoa
vitambulisho vya taifa kwa wananchi wakati Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi Mh. Mathias Chikawe alipotembelea Mabanda ya Wizara yake
katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269