Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar es Salaam.
Safari
ya Kutafuta vipaji katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT)
ilianzia Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza ambapo timu nzima ya TMT ilikuwa
katika kanda hiyo kwaajili ya kusaka vipaji kupitia shindano hilo kubwa
na la kwanza kufanyika Afrika Mashariki na Kati.
Shindano la Tanzania Movie Talents ni shindano ambalo lilizunguka kanda zote sita za Tanzania na hatimaye kilele chake kilimalizika mnamo tarehe 18 Juni 2014 katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam katika Ukanda wa Pwani na kupelekea washindi watano kupatikana na kukabidhiwa Shilingi laki tano kila Mmoja.
Shindano la Tanzania Movie Talents ni shindano ambalo lilizunguka kanda zote sita za Tanzania na hatimaye kilele chake kilimalizika mnamo tarehe 18 Juni 2014 katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam katika Ukanda wa Pwani na kupelekea washindi watano kupatikana na kukabidhiwa Shilingi laki tano kila Mmoja.
Mara
baada ya kumalizika kwa hatua ya kwanza ya kutafuta washindi kutoka
kanda zote sita sasa ni wakati wa washindi wa kanda hizo kuja jijini Dar
es Salaam na Kukaa kambi moja huku wakipatiwa mafunzo kutoka kwa Walimu
wa Sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo
lengo likiwa ni kuwapika kisanaa na kuanza kushindanishwa ili kuweza
kupata Mshindi mmoja ambaye ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50
katika fainali itakayofanyika mwisho wa Mwezi wa nane Jijini Dar Es
Salaam.
Mara
baada ya Fainali hiyo kumaliza washindi kumi watakaopatikana watakuwa
chini ya Kampuni ya Proin Promotions na wataweza kutengeneza filamu ya
Pamoja na hatimaye kuja kunufaika na filamu hiyo.
Shindano
la TMT limekuwa ni shindano kubwa kabisa ambalo halijawahi kufanyika
nchini na limekuwa likirusha vipindi vyake katika kituo cha Runinga cha
ITV kuanzia mida ya Saa Nne Usiku siku ya Jumamosi na Marudio yake ni
Kila Jumapili Saa 10 Jioni na Jumatano Saa 5 usiku huku Jumamosi ya
tarehe 21 Juni 2014 kipindi cha Dar Es Salaam kitarushwa kupitia kituo
hiko cha runinga na hatimaye Kazi ya Mchujo Kuanza Mara moja mara baada
ya washindi wa kanda zote kuwasili Jijini Dar Es Salaam na kuanza kambi
huku wananchi watakuwa wakiwapigia kura washiriki ambao wanawaona wenye
uwezo.
Wafanyakazi
wa Kampuni ya Proin Promotions katika Mradi wa Kusaka vipaji vya
Kuigiza Nchini TMT (Tanzania Movie Talents) wakishangilia kwa kufungua
Mvinyo usio na kilevi mara baada ya kumaliza zoezi la Kuzunguka Katika
Kanda Sita nchini kwa kusaka Vipaji vya kuigiza ambapo zoezi hilo
lilimalizika katika Kanda ya Pwani, Mkoani Dar Es Salaam ambapo washindi
watano kutoka kanda ya Pwani walipatikana na Kupewa zawadi zao za
Shilingi laki Tano Kila Mmoja na Kushiriki katika fainali ya Kuwania
Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Mmoja
wa Majaji katika Shindano la TMT Yvonne Cherry au Monalisa akifurahia
kufungua Mvinyo huku wafanyakazi wa Proin wakifurahia pia kwa kukinga
mvinyo huo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kusaka vipaji vya
kuigiza katika Kanda ya Pwani ambapo ndio imefunga zoezi hilo
lililoanzia Kanda ya Ziwa, Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na
Kaskazini.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya Proin Group of Companies,Bw Johnson Lukaza akiongea na
wafanyakazi wa Proin Promotions limited mara baada ya kumaliza vizuri
kwa kazi za kutafuta vipaji katika Kanda Sita za Tanzania.Pamoja na
kuongea na wafanyakazi hao aliweza kutoa neno la shukrani kwa kila mmoja
kwa kutimiza wajibu wake na hatimaye kufanikisha zoezi hilo la hatua ya
kwanza kumalizika vyema.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269