Breaking News

Your Ad Spot

Jun 23, 2014

NEHEMIA MCHECHU ATEULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA SERENGETI BREWERIES LTD (SBL).

Kampuni ya Serengeti Breweries Limited ( SBL ) leo inatangaza uteuzi wa Ndugu Nehemia Mchechu kama Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya SBL
Uteuzi wa Ndugu Mchechu unafuata ukamilisho wa umiliki wa Mhe. Jaji (mstaafu) Mark Bomani . Katika nafasi yake mpya , Bw Mchechu pia atakukwa memba wa bodi ya  kampuni ya bia ya East Africa.
Ndugu,Nehemia Mchechu kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba la Taifa ( NHC) . Bw. Mchechu anauzoefu mkubwa katika masuala ya fedha na usimamizi. Hapo awali alishika  nafasi muhimu katika sekta ya benki , hasa kama Mkuu wa Masoko Kimataifa na mkurugenzi msaidizi benki ya Standard Chartered, na  kuwa Mkurugenzi Mtendaji  benki ya  Commercial Bank of Africa Tanzania (CBA) .
Bwa.Mchechu ana Shahada ya Biashara (Fedha) na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Yeye pia ni Rais wa Umoja wa wanafunzi waliomaliza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Biashara na mwanachama wa ACI – Financial Market Association Tanzania.
Miongoni mwa nafasi nyingine muhimu, Bwa.Mchechu pia ni Mkurugenzi na mwanachama wa CEORT na  pia ni Mkurugenzii wa TIC.
SBL inachukua fursa hii kumkaribisha na kumpongeza Mwenyekiti wake mpya wa bodi na kuwashukuru mwenyekiti wa bodi Mheshimiwa Bomani kwa mchango wake bora na wa kipekee wakati wa uongozi wake.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages