Breaking News

Your Ad Spot

Jun 29, 2014

TAMWA KUPAMBANA NA ULEVI WA KUPINDUKIA

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka akisisitiza jambo katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka akisisitiza jambo katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leoMkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na TAMWA ukiendelea. Mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na TAMWA ukiendeleaBaadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo.Sehemu ya wahariri wa vyombo anuai vya habari jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka (hayupo pichani). Sehemu ya wahariri wa vyombo anuai vya habari jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka (hayupo pichani).Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leoBaadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo.

 KITUO cha Usuluhishi (CRC) kinachofanya kazi chini ya Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) kimejipanga kutoa elimu kwa jamii kuhakikisha kinapambana na matumizi ya pombe kupindukia kwa jamii suala ambalo limezidisha vitendo vya ukatili wa jinsia unaofanywa na watumiaji pombe kupindukia.

 Akizungumza na wahariri wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka alisema utafiti uliofanywa na Shirika la IOGT International unaonesha kuwa kiwango cha unywaji pombe jijini Dar es Salaam ni asilimia 47.6 kwa wanaume na asilimia 29 kwa wanawake huku ikibainika kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya vitendo vya ukatili na matumizi ya pombe kupita kiasi.

 Bi. Soka alisema takwimu zinaonesha kuwa wanawake ambao waume zao wanalewa mara kwa mara wengi wao wanakumbana na ukatili unaohusisha vipigo, kuumizwa na ukatili wa kingono kwa asilimia 77, huku kiwango cha ukatili kwa wanawake ambao waume ama wenzi wao hawanywi pombe ni asilimia 33.

 "...Utafiti uliofanywa na shirika la IOGT International unaonyesha kwamba kiwango cha unywaji pombe katika jiji la Dar es Salaam ni asilimia 47.6 kwa wanaume na asilimia 29 kwa wanawake...lakini takwimu kutokana na utafiti wa Demographia na Afya Tanzania (TDHS) 2010...unaonesha wanawake ambao waume zao wanalewa mara kwa mara wengi wao wanakumbana na ukatili unaohusisha kipigo/kuumizwa na ukatili wa kingono kwa asilimia 77," alisema.

 Aidha aliviomba vyombo vya habari kushirikiana na TAMWA kutoa elimu kwa jamii kupunguza matumizi ya pombe kupindukia kwani licha ya ukatili huo familia pia zimekuwa zikiathirika kiuchumi juu ya matumizi ya pombe huku baadhi ya watoto wakikosa huduma za msingi kutoka kwa baadhi ya wazazi ambao ni walevi kupindukia.

 Alisema TAMWA inatekeleza mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana unaosababishwa na pombe huku lengo kuu ikiwa ni kuhakikisha maisha ya wanawake na watoto yanaboreshwa kwa kuimarisha sheria na kupunguza ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupindukia.

Hata hivyo alisema tayari chama hicho kimeanza kufanya utafiti mwingine katika Wilaya ya Kinondoni kuangalia madhara yanayotokana na unywaji wa pombe kupindukia ili kuangalia hali halisi ya matumizi ya pombe eneo hilo na madhara ambayo yamekuwa yakitokana na matumizi hayo.

Alisema malengo mengine ya mradi ni pamoja na kuboresha maisha ya wanawake na watoto kwa kuimarisha sheria na kupunguza ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe katika wilaya ya Kinondoni na pia kujenga uelewa miongoni mwa jamii juu ya madhara yatokanayo na unywaji wa pombe kupindukia.

 Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA aliongeza kuwa mapambano hayo pia yatasaidia, kukabiliana na matumizi ya pombe na kutoa taarifa kwa vyombo husika kuhusu ukatili dhidi ya wanawake unaotokana na matumizi ya pombe, ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo wa jamii kukabiliana na ukatili unaosababishwa na unywaji wa pombe dhidi ya wanawake na watoto. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages