Na Sylvester Onesmo
wa Jeshi la Polisi, Dodoma.
Watu wawili wamepoteza maisha kutokana na ajali mbili zilizotokea katika maeneo mawili tofauti na nyakati tofauti Mkoani Dodoma.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME – SACP (pichani) ameeleza kuwa, ajali ya kwanza ilitokea tarehe
30/05/2014 majira ya saa 18:30hrs katika kijiji cha Ipala Wilaya ya
Dodoma ambapo gari lenye namba za usajili DFP 614 Toyota Land Cruiser
mali ya chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo likitokea chuoni kuelekea
Dodoma mjini likiendeshwa na ALFRED S/O MLIGO, MIAKA 35, MHEHE, liliacha
njia na kupinduka na kusababisha kifo chake. Pia watu watano walipata
maumivu mbalimbali na walitibiwa na kuruhusiwa.
Mwili wa marehemu upo katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma kusubiri taratibu nyingine.
Kamanda
MISIME AMESEMA ajali ya pili imetokea majira ya saa 18:45hrs huko
katika kijiji cha SILWA barabara ya Dodoma – Morogoro ambapo gari lenye
namba za usajili T.150 CWA Toyota Granvia Station Wagon likiendeshwa na
MGENI S/O SHEMAKAME, MBONDEI, MIAKA 29 MKAZI WA MBURAHATI DSM liliacha
njia na kusababisha kifo cha GEORGE S/O TYSON, MIAKA 39, MWANAHABARI,
Mkazi wa mbezi DSM.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo ukisubiri taratibu za Polisi na wanandugu.
Pia katika ajali hiyo wanahabari wanne (4) wa Mboni show walipata majeraha mbalimbali na kutibiwa na kuruhusiwa, ambao ni:-
1. NIXON S/O KABUMBILE, MHAYA, MIAKA 31
2. GRACE D/O MEENA, MCHAGA, MIAKA 28
3. NTWA S/O KABOLE, MNYAKYUSA, MIAKA 33
4. JUSTINE S/O BAYO, MIAKA 27, MMASAI
Uchunguzi
wa awali unaonyesha ajali zote mbili zimesababishwa na
mwendokasi. Kamanda MISIME ametoa wito kwa madereva kuepuka mwendokasi
na kuwa na udereva wa kujihami ambao unasaidia dereva kusimama bila
kusababisha madhara linapotokea jambo lolote na hata kama ajali ikitokea
madhara hayawezi kuwa makubwa kama yanavyokuwa anapokuwa kwenye mwendo
wa kasi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269