Kutoka kushoto ni Bw. Steven Smith, Bi Ann Hanin, Mhe. Balozi Tuvako Manongi na Bibi Judith Smith
NA MWADISHI WETU, NEWYORK
Baada ya kuridhishwa na matumizi mazuri na mafanikio
makubwa ya Maktaba yao ya kwanza waliyoifungua mwaka 2009 katika
kijiji cha Ngongongare Mkoani Arusha.
Taasisis isiyo ya kiserikali
ya The Crawford Smith Foundation yenye makazi yake nchini Marekani
na ambayo ndiyo inayosimamia mradi wa uanzishwa na uendeshaji wa
Maktaba hususani katika maeneo ya vijijini, sasa inakusudia kujenga
maktaba nyingine sita katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Maktaba
hiyo ya kwanza na ya aina yake na ambayo imepewa jina la Jifundishe
Free Library, si tu inatoa huduma za vitabu vya kiada na ziada kwa
watumiaji ambao ni kuanzia wale wa shule za awali, msingi, sekondari na
hata vyuo vikuu, bali pia imekuwa kituo ambacho kinawasaidia
wanawake na vijana kujifunza stadi mbalimbali zikiwamo za
ujasiliamali, vyama ya kuweka na kukopa, huduma za kinga ya afya,
huduma za internet na mafunzo ya ziada ambayo yamekuwa yakitolewa na
wataalamu wa kujitolea kutoka nje na ndani ya Tanzania.
Hayo
yameelewa na Viongozi wakuu wa Taasisi hiyo ya The Crasford Smith
Foundation wakati walipofika na kufanya Mazungumzo na Balozi Tuvako
Manongi Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Kwa
mujibu wa maelezo ya Bw. Steven Smith aliyekuwa amefuatana na Mke
wake Bibi. Judithi Smith amesema kuwa mwitikio mkubwa na matumizi
sahihi na endelevu vya Jifundishe Free Library na matokeo mazuri ya
wanafunzi katika mitihani yao, kumewafanya watambue ni kwa kiasi gani
huduma hiyo muhimu inahitaji kusambazwa katika maeneo mengine hasa
ya vijijini. Lengo likiwa ni kuwafikia na kuwapatia huduma hiyo wasio
kuwa na uwezo wa kuipata kwa urahisi.
Mradi huo wa Maktaba
licha ya kutoa huduma mbalimbali, lakini umekwenda mbali zaidi kwa
kutoa ufadhili wa masomo ya Chuo Kikuu kwa wanafunzi wanne hadi sasa.
baadhi ya wanafunzi hao wamerudi na kutoa mchango wao katika Maktaba
hiyo na jumuiya inayoizunguka.
Baadhi ya maeneo ambako
wanakusudia kupelea huduma hiyo muhimu ya maktaba ni Kisarawe , Chunya , Iringa, Morogoro na Kilimanjaro. Aidha wakuu hao
wameeleza kuridhidhwa kwao na Ushirikiano wanaoupata kutoka kwa
viongozi mbalimbali wa Serikali akiwamo Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
baadhi ya Makampuni ambayo yameonyesha nia ya kushirikia na Taasisi
hiyo katika utoaji wa huduma hiyo, na vilevile mwamko na moyo
wakujitolea wa watanzania katika maeneo wanayokusudia kuanzisha
maktaba hizo.
Kwa upande wake, Mhe. Balozi Balozi Manongi
aliishukuru Taasisi hiyo kwa mchango wake mkubwa na ambao umeonyesha
mafanikio na mabadiliko makubwa kwa jamii inayohudumiwa. Akasema
Tanzania inatambua umuhimu wa maktaba katika mustakabali mzima wa elimu
na mafunzo na kwamba mchango wa taasisi zisizo za kiserikali
unakaribishwa sana.
Your Ad Spot
Jul 25, 2014
Home
Unlabelled
CRAWFORD SMITH FOUNDATION YAKUSUDIA KUSAMBAZA HUDUMA YA MAKTABA KWA WENGI
CRAWFORD SMITH FOUNDATION YAKUSUDIA KUSAMBAZA HUDUMA YA MAKTABA KWA WENGI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269